Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Alkhamisi, 30 Oktoba 2014 11:17

Kipindi maalumu cha mahojiano ya Muharram

Kipindi maalumu cha mahojiano ya Muharram

Bismillahir Rahmanir Rahim. Maadhimisho ya Muharram na mapambano ya Imam Husain AS yamekuwa yakiongeza nuru yake katika maeneo tofauti duniani, siku baada ya siku.

Hayo yalikuwa ni mapambano ambayo damu iliushinda upanga. Yalikuwa ni mapambano ya kishujaa ambayo, kadiri siku zinavyopita na kadiri karne zinavyobadilika ndivyo athari zake zinavyozidi kuzitia nguvu nyoyo za wapigania haki duniani.

Ushahidi wa kihistoria unathibitisha kuwa mapambano ya Imam Husain AS huko Karbala hayakuziathiri nyoyo za wapenzi wa Ahlul Bayt na Waislamu peke yake, bali yamefanywa kigezo pia na hata wasiokuwa Waislamu kama vile shujaa wa India na baba wa taifa hilo, Mohandas Karamchand Gandhi maarufu kwa jina la Mahatma Ghandhi ambaye alinukuliwa akitoa matamshi mazuri sana kuhusu namna alivyoathirika na mapambano ya Imam Husain AS.

Hapa chini tumekuwekeeni kipindi maalumu cha mahojiano ambayo ndani yake tumewahoji Bw. Abbas Ali wa Lamu nchini Kenya pamoja na Bw. Salim Ramadhani na Bi Zuleikha Hussein wa mkoani Tanga Tanzania.

Ingia hapa chini kusikiliza kipindi hicho

Sauti na Video

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …