Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Ijumaa, 06 Novemba 2015 08:49

Filamu ya Muhammad, (saw) yaonyeshwa Lebanon

Filamu ya Muhammad, (saw) yaonyeshwa Lebanon

Filamu ya Muhammad Rasulullah" ambayo ndiyo kubwa zaidi iliyowahi kutengenezwa katika ulimwengu wa Kiislamu ilionyeshwa jana kwa mara ya kwanza nchini Lebanon.
Filamu hiyo ya Muhammad, Mtume wa Mwenyezi Mungu ambayo imetengenezwa nchini Iran imeonyeshwa katika ukumbi uliojumuisha maulama wa Kisuni na Kishia, shakhsia wa kiutamaduni na kisanaa wa Lebanon. Katika miezi ya hivi karibuni filamu hiyo imeshambuliwa na baadhi ya ya maulama walioathiriwa na propaganda chafu wa Saudi Arabia na al Azhar nchini Misri.
Sheikh Mahmoud Mahir ambaye ni Mufti wa mji wa Saida (Sidon) nchini Lebanon amesema baada ya kutazama filamu hiyo kwamba ni athari kubwa ambayo ndani yake kumefanyika jitihada kabambe na yenye taathira nyingi.
Kwa upande wake Sheikh Waliid Allamah ambaye ni mufti wa Ahlusunna na miongoni mwa maafisa wa Harakati ya Amal al Islami ya Lebanon amesema kuhusu filamu ya Muhammad Rasulullah kwamba filamu hiyo inamuathiri mtazamaji wake kwa kadiri kwamba analazimika kushikilia pumzi kifuani na kububujikwa na machozi.
Filamu ya Muhammad Rasulullah iliyotengenezwa hapa nchini na mtengeneza filamu mashuhuri Majid Majidi inasimulia maisha ya Mtume Muhammad (saw) katika kipindi cha utotoni mwake.
Filamu hiyo yenye dakika 171 imetengenezwa kwa bajeti ya dola milioni 50 na imetajwa kuwa filamu iliyogharimu kiasi kikubwa zaidi cha fedha nchini Iran na utengenezaji wake umechukua kipindi cha miaka mitano.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …