Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumanne, 03 Februari 2015 15:55

Uislamu na Mtindo wa Maisha (54)

Uislamu na Mtindo wa Maisha (54)

Ni wakati wingine wa kuwa nanyi wafuatiliaji wa kipindi hiki cha Uislamu na Mtindo wa Maisha. Kama bado mnakumbuka katika vipindi kadhaa vilivyopita tulizungumzia uhusiano wa mke na mume ndani ya familia katika mtindo wa maisha wa Kiislamu na vilevile malezi ya watoto hususan malezi ya kidini. Wiki hii tutazungumzia kipindi nyeti na muhimu sana cha ubarubaro na wanawari na jinsi ya kuamiliana na watoto wenye rika hilo ndani ya familia.

Kipindi cha ubarubaro na uanawari ni kipindi muhimu sana katika maisha ya kila mtu. Kipindi hicho ni kile kilichopo baina ya utoto na utu uzima na katika kipindi hicho mwanadamu hupatwa na mabadiliko ya haraka ya kimwili na kiroho. Kwa msingi huo huambatana na migongano mingi baina ya dunia hizo mbili yaani dunia ya utoto na ile ya utu uzima.
Barubaru na mwanamwari hufanya jitihada za kupata utambulisho wake halisi na hutumia kila fursa kuthibitisha dhati yake na kudhihirisha uwezo wake. Kipindi cha ubarubaru ni kipindi cha mtu kuachana na zama za kuwa tegemezi kwa familia na wazazi wawili na kuingia katika medani ya jamii.
Awali kabisa tunapaswa kusema kuwa, wazazi wawili hawapasi kuwafanya watoto kuwa tegemezi kupita kiasi ili waweze kuwatayarishia uwanja mzuri wa wepesi wa kujitegemea. Vilevile wazazi wanaweza kumfanya mtoto aridhike na nafsi yake kwa kiwango fulani kwa kumpa fursa ya kujitegemea katika baadhi ya mambo. Hii ni kwa sababu barubaru na mwanamwali ambaye shakhsia yake inaheshimiwa na kuthaminiwa ndani ya familia na ambaye huwa mwanachama mwenye taathira ndani ya taasisi hiyo, huwa mwenye utulivu kiroho na kinafsi. Kutokana na kujiamini kwake, kijana kama huyu huwa hajihisi hakiri na duni au kuwa na nakisi na kasoro. Imam Ali bin Abi Twalib (as) anasema: Mtu anayeamini sharafu yake ya kiroho na utukufu wake wa kinafsi huwa hadhalilishi nafsi yake kwa kufanya madhambi na mambo maovu".
Wazazi wawili wanapaswa kufanya jitihada kuhakikisha kwamba, kijana wao anapata hali ya kujiamini na vilevile kuwa na hisi ya kuridhika ndani ya nafsi yake. Wataalamu wa elimu nafsi wanasema miongoni mwa mambo yenye taathira kubwa katika kuboresha uhusiano wa wazazi wawili na watoto wao hususan vijana ni kuimarisha hisi ya kujiona kuwa wanathaminiwa na hisi ya kujiamini ndani ya nafsi zao. Wataalamu hao wanawausia wazazi wawili kusifia uwezo wa vijana na kuwaimarisha bila kutia chumvi au kuchupa mipaka ya kawaida katika suala hilo.
Kipindi cha ubarubaru na ujana ni kipindi cha kuhama kutoka utotoni na kuingia katika utu uzima. Katika safari hiyo ya kuhama, barubaru na mwanamwari hufanya jitihada za kujioanisha na kwenda sambamba na mazingira mapya. Kiwango cha mafanikio yake katika kuvuka kipindi hiki cha mpito hufungamana na kiwango cha utayarifu wake kwa ajili ya kipindi hicho. Ustawi mzuri wa kinafsi ni miongoni mwa sababu muhimu sana katika kumuwezesha kijana kuwiana na kwenda sawa na mazingira hayo. Kwa maneno mengine ni kuwa, utayarifu wa kiroho na kinafsi wa kijana humsaidia katika kwenda sambamba na mabadiliko yanayojitokeza.
Katika kipindi hiki kijana hukumbana na mabadiliko mengi ya kiroho na kijamii. Wakati huo utiifu wa kijana kwa wazazi wawili huanza kupungua hatua kwa hatua, na zaidi hujielekeza kwa vijana wa rika na umri wake. Wakati huo hutaka kuwaonesha kuwa ni mtu huru na anayejitegemea.
Jambo jingine linalojitokeza katika kipindi hiki cha ubarubaru na ujana ni kushadidi jazba na mihemko yake. Barubaru na vijana hupatwa na hasira kali, kukata tamaa haraka na kupatwa na woga na hofu. Wakati huu yumkini baadhi ya vijana wakafanya mambo yasiyo ya kawaida kutokana na mihemko na jazba na vilevile kutojua jinsi ya kudhihirisha hisia zao. Mara nyingine vijana hushindwa kuwa macho na tahadhari kuhusu mienendo na hisia zao. Suala hili huwapelekea kufanya mambo ya haraka haraka na yasiyopimwa. Wataalamu wa elimu nafsi wanasema ubarubaru na ujana ni kipindi cha kukusanya tajiriba na uzoefu kwa ajili ya kuanza kujitegemea kiroho na kijamii. Kama atavuka kipindi hiki kwa mafanikio basi atakuwa na mustakbali mwema, la sivyo asilimia ya kukumbana na matatizo katika kipindi cha ujana itakuwa kubwa. Katika kipindi hiki pia aghlabu, vijana ndipo huanza kutumbukia katika uhalifu, upotofu, dawa za kulevya na kadhalika. >
Kipindi cha ubarubaru na ujana kina panda shuka na misukusuko mingi. Kwa msingi huo wazazi wanaweza kumsaidia kijana kuvuka vyema kipindi hiki kwa kutilia maanani na kujali ipasavyo hisia na matakwa yake. Usimamizi na miongozo ya wazazi wawili inapaswa kuwa kama tochi inayomulika katika anga yenye giza na kiwingu na kumwonesha kijana njia sahihi katika kipindi chote cha balehe na ujana. Vijana huwa na mahitaji ya kimwili, kiroho, kifikra na kidini, hivyo humtaka baba au mama kwa njia ya moja kwa moja au isiyo ya moja kwa moja, kujibu na kukidhi matakwa hayo. Miongoni mwa mambo ya dharura sana ya kipindi hiki ni malezi ya kidini na kama bado mnakumbuka, tulizungumzia suala hilo katika vipindi kadhaa vilivyopita. Hata hivyo tunaona udharura wa kuashiria tena baadhi ya nukta muhimu kuhusu malezi ya kidini ya vijana:
Kama mnavyojua, fikra za kidini na hamu ya vijana kwa maadili bora vinaweza kustawi na kuchanua katika kipindi cha ujana. Baadhi ya barubaru na vijana hupendelea kuona si wao pekee bali hata matendo na mienendo ya vijana wenzao yakifuata maslahi, kheri na njia sahihi. Fikra kama hizi humwepusha kijana kutumbukia katika upotofu na kumuweka mbali na ufuska. Japokuwa kipindi cha ujana na ubarubaru huandamana na usafi wa roho lakini pia huwa kipindi cha kujitokeza shaka ndani ya akili na nafsi ya kijana kuhusu masuala mengi hususan yale ya kidini. Wakati mwingine kijana huanza kuwa na shaka kuhusu itikadi zake na za wazazi wake na kutaka kuwa na yakini kwamba yale aliyoyaamini ni sahihi au la. Katika kipindi hiki hutaka kukubali au kukataa itikadi zake kwa kutimia hoja za kimantiki na kiakili na vilevile hutaka kupata tafsiri mpya kuhusu itikadi na imani zake. Wakati mwingine kijana huwa na wasiwasi wa kuzungumzia shaka na dukuduku zake za kiitikadi mbele ya watu wengine na hapa ndipo unapotokea mushkeli na tatizo kwamba yumkini kijana akabakia na shaka hizo bila ya kupata majibu sahihi. Hatari nyingine ni kwamba yumkini kijana huyu akaelekea kwa watu wasiostahiki na wasio wema kwa ajili ya kuondoa shaka na dukuduku zake kuhusu masuala ya kidini.
Kwa msingi huo wazazi wawili, walimu na walezi wana nafasi kubwa na muhimu sana katika kumuongoza kijana na barubaru na kumuelekeza kwenye misingi ya dini na maadili mema. Uhusiano wa kimafunzo na kidini wa wazazi na walezi pamoja na vijana unapaswa kuwa wa kirafiki, upendo na kwa mujibu wa hoja za kimantiki. Vijana wanapaswa kufundishwa njia sahihi za kutafakari, na itikadi ya Tauhidi na misingi mingine ya dini inapaswa kuelezwa kwa vijana kwa buruhani na njia za kimantiki. Katika uwanja huu pia wazazi wanaweza kuwaelekeza na kuwahamasisha vijana kusoma vitabu vinavyofaa na vinavyoweza kujibu dukuduku na maswali yao ya kiitikadi. Pamoja na hayo tunapaswa kuelewa kuwa, mbinu ya kuuliza maswali na kujadili masuala ya kidini na vijana ndiyo yenye umuhimu na taathira kubwa zaidi. Maudhui za kidini zinapaswa kubainishwa kwa njia ambayo masuala ya kidini yataoana na maisha yao ya kila siku. Vijana wanapaswa kuhisi kuwa masuala ya kidini yana taathira chanya katika maisha yao ya kila siku na yanaweza kukidhi mahitaji yao ya kiroho.
Malezi sahihi na miongozo ya wazazi na walezi inaweza kuwafikisha vijana katika imani kwamba dini inaoana kikamilifi na akili na mantiki. Wakati huo kijana ataelewa kuwa katika dunia ya leo ambapo sayansi, elimu na teknolojia vinakwenda kwa kasi kubwa, dini na mafundisho yake si kizuizi bali vinamsaidia mwanadamu katika uwanja huo na kumwonesha njia ya kustafidi

 

 

 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)