Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumanne, 22 Septemba 2015 15:52

Dondoo za Hija (10)

Dondoo za Hija (10)

Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh. Leo tarehe 10 Dhulhija ni sikukuu ya Idul Adh'ha. Adil Adh'ha ni sikukuu ya kujikomboa mwanadamu na sikukuu ya imani na kumpenda haswa Mwenyezi Mungu SW. Siku hii inakumbusha ikhlasi ya kweli na Nabii Ibrahim (as) kwa Mola wake Muumba. Katika siku hii mahujaji wa Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu huelekea Mina kwa shauku kubwa na kuibua tena kumbukumbu ya imani na kujisalimisha kikamilifu kwa Mtume adhimu aliyekumbana na mtihani mkubwa na nzito. Baada ya kuona ndoto ya kweli akiamrishwa kumchinja mwanaye kipenzi Ismail, mja mwema wa Mwenyezi Mungu Ibrahim Khalilullah alijitayarisha kuchinja shingo la mtoto wake baada ya mapambano makali ya ndani ya nafsi yake. Hata hivyo wakati alipomlaza chini mwanaye kumchinja na baada ya Mwenezi Mungu kuelewa kwamba mja wake mwema Nabii Ibrahim ameshinda mtihani kwa kuchinja matakwa na mapenzi yake, alimtuma kondoo kwa Mtume Wake huyo na hapohapo ilisikika sauti kutoka mbinguni ikisema: Hakika umeshinda mtihani ewe Ibrahim.
Baada ya kuvuka milima na mabonde na shaka na mivutano ya ndani ya nafsi kutokana na kutakiwa kumchinja mwanaye kipenzi, Nabii Ibrahim aliingia katika ago ya imani na yaqini na kusafisha nafsi yake katika zamzam na maji ya upendo, mahaba na kumpenda Mwenyezi Mungu kuliko mambo yote mengine. Tangu siku hiyo ilifaradhishwa amali ya kuchinja mnyama huko Mina na siku hiyo ikaainishwa kuwa ni siku ya idi na sikukuu. Siku hii mamilioni ya mahujaji wanaharakia kutufu Nyumba ya Mwenyezi Mungu na baadaye huelekea Mina na kutekeleza amali zinazotakiwa kufanywa huko ikiwa ni pamoja na kuchinja mnyama wa sadaka. Kuchinja ng'ombe, kondoo au ngamia kwa wenye kuhiji ni ishara ya kuchinja na kukata kabisa matamanio na matakwa ya nafsi na ya kimaada mbele ya amri na matakwa ya Mwenyezi Mungu. Mjukuu wa Mtume wetu Muhammad (saw) Imam Jaafar Swadiq anasema: Unapotaka kuchinja mnyama wa sadaka katika ibada ya Hija muelekeze kibla kisha sema: Swala na sadaka yangu, kifo na uhai wangu vyote ni vya Mwenyezi Mungu pekee Muumba wa ulimwengu na vilivyomo. Tunakutakieni nyote sikukuu njema. Wassalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …