Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumanne, 22 Septemba 2015 15:51

Dondoo za Hija (9)

Dondoo za Hija (9)

Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh. Kandokando ya Al Kaaba kuna kijiduara kinachoitwa Hijr Ismail ambako ndipo lilipo kaburi la Hajar mkee wa Nabii Ibrahim al Khalil, Nabii Ismail na Mitume wengine wengi wa Mwenyezi Mungu. Mtu anayefanya twawafu na kuzunguka al Kaaba anawajibika pia kutufu Hijr Ismail. Maana ya harakati hii ni kwamba tunapaswa kuwa mithili ya Bibi Hajar na Ismail na tufanye jitihada kubwa za kumridhisha Mwenyezi Mungu kama wao walivyosabilia maisha yao kwa ajili ya kupata radhi za Allah SW.
Miongoni mwa adabu na taratibu za ibada ya Hija ni kwamba wakati tunapotufu na kuzunguka al Kaaba, bega letu la kushoto linapaswa kuwa limeeleka upande wa Nyumba hiyo ya Mwenyezi Mungu. Jambo la kuvutia hapa ni kuwa, moyo wa mwandamu pia uko upande wake wa kushoto. Hivyo basi kuwepo moyo wa mwanadamu upande unaoelekea na kukaribia al Kaaba kuna maana ya kusalimisha moyo kwa Mola wa al Kaaba.
Mmoja kati ya watu waliosilimu na kukhitari dini ya Uislamu hivi karibuni ameandika katika kumbukumbu zake za safari ya Hija kwamba: Sikuamini macho yangu. Nilikuwa nimeketi nikiangalia eneo tukufu kuliko yote duniani. Allahu Akbar! Nilikuwa nikiangalia nyumba ambayo ndiyo kitovu cha mazingatio ya mamilioni ya watu. Nilikuwa nikiwaza na kuwazua, nyumba na kimya chake hiki kina siri gani? Subhanallah! Nilikuwa hatua kadhaa tu kutoka kwenye kituo ambacho kila siku mamilioni ya watu duniani huswali wakielekea upande wake. Sifa kubwa zaidi ya nyumba hiyo ni kwamba watu wote kandokando yake wanajihisi kuwa na utulivu na amani. Nilikuwa na hisia isiyoweza kusifika.. Hapo kandokando ya al Kaaba nilitambua zaidi kuwa Mwenyezi Mungu ni muweza wa kila kitu na rehma zake zimeenea kila mahali. Wema wake hauna mpaka na sisi wanadamu tunaogelea katika bahari ya rehma na neema zake. Wassalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …