Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumanne, 22 Septemba 2015 15:22

Dondoo za Hija (8)

Dondoo za Hija (8)

Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh. Katibuni katika mfululizo wa vipindi vyetu vifupi vya Dondoo za Hija, leo tutaangazia moja ya mawaqif za Hija.
Mwenye kuhiji anapaswa kusimama maeneo matatu. Anasimama Arafat, Mashaar na Minaa. Arafat ni eneo lililo kaskazini mwa Makka katika safu ya mlima ujulikanao kama Jabal ar-Rahma. Arafat ni ardhi takatifu ambapo Mwenyezi Mungu amewataka wafanya ziara katika nyumba yake wafike na kusimama hapo kwa pamoja katika wakati maalumu. Kila moja mwenye kusimama hapo ajitahidi kwa uwezi wake kunufaika na rahma za Mola Muumba. Arafat ni eneo la la kutambua na kutafakari. Kutambua na kuwa macho katika maisha ni siri ya mafanikio. Mwanadamu anapaswa kuchukua tahadhari kuhusu nyadhifa na majukumu yake maishani. Awe macho kuhusu matukio ambayo yanaweza kutoa pigo kwa roho yake. Kwa hivyo msingi wa kuwa macho na kuchukua tahhadhari sambamba na uono wa mbali ni nukta zinazozingatiwa sana katika mafundisho ya Kiislamu. Mwanadamu anapaswa kuwa na tadibiri kuhusu matukio yanayojiri na yanayotazamiwa kujiri ili aweze kupata maarifa na kuchukua tahadhari. Imam Ali AS alisema: "Rehema za Mwenyezi Mungu zinamshukia mtu ambayo anatafakari na kwa msingi kuwa kupima mambo." Thamani ya uelewa huu pamoja na uono wa mbali imebainika katika riwaya isemayo: "Hakuna mtu Muumini kutoka kila kijiji au mji anayesimama Arafat ila Mwenyezi Mungu huwasamehe wakaazi wa eneo lake na wala hakuna mtu Muumini, kutoka familia ya watu wenye imani, anayesimama Arafat ila Mwenyezi Mungu huwasamewe hamaa zake wenye iamani."
Katika Hija ya Mwisho ya Mtume SAW, alipohitimisha kisimamo chake, Arafat, Mtukufu huyo alimwambia Mwadhini wake, Bilal kuwa: "Ewe Bilal! Waambie watu watulie. Baada ya wote kunyamaza kimya, Rasulullah SAW alisema: "Yule yule Mola Wenu Ambaye leo Amewarehemu, pia Amewasamehe wema miongoni mwenu ...na kuwapa haki ya shifaa kwa wasiowema. Amewasamehe waovu kwa shifaa ya waliowema. Sasa munaneda katika hali ambayo kwa ujumla mumesamehewa na mumepata maghfira na Msamaha wa Mwenyezi Mungu.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …