Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatatu, 21 Septemba 2015 18:47

Dondoo za Hija (7)

Dondoo za Hija (7)

Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh. Leo ni tarehe 7 Dhulhijjah. Katika utamaduni wa Uislamu wapenzi wasikilizaji, kiini cha ibada kiroho ni kumuelekea Mwenyezi Mungu, na kiini chake cha siasa ni kuwajali waja wa Mwenyezi Mungu. Mawili haya yamechanganyika pamoja katika Hija mithili ya roho na kiwiliwili! Hija kwa upande mmoja ni kujenga mazoea na mawasiliano kwa ikhlasi na Mwenyezi Mungu, na kwa upande mwengine ni wenzo wa mawasiliano na kuleta umoja katika safu za Waislamu. Wakati tazamo la wafanyaziara wote linapoelekezwa kwenye kitovu kimoja kikuu, huvipa mgongo vyanzo bandia vya nguvu, na ambavyo si lolote si chochote mbele ya nguvu na adhama ya Mwenyezi Mungu. Hisi hii ya pamoja huwezesha Waislamu kujenga nguvu ya pamoja na kuundwa chombo kimoja cha kisiasa kilicho imara na chenye nguvu katika umma wa Kiislamu. Katika mjumuiko wenye adhama kubwa wa Hija, Waislamu hupata taarifa za kisiasa za nchi za Kiislamu za kila pembe ya dunia na kuvunja uzio wa ubanaji taarifa na kutokomeza hali kandamizi iliyojengwa na mifumo ya kidhalimu inayotawala katika nchi za Kiislamu. Katika zile zama ambapo watawala majabari wakiwemo wa Bani Umayyah na Bani Abbas walipokuwa wakitawala ardhi tukufu za Kiislamu na kudhibiti kila aina ya mawasiliano baina ya Waislamu ili kuweza kuzima harakati yoyote ile ya kujikomboa, kuwadia msimu wa Hija kulitoa upenyo wa kuwasiliana watu wa matabaka tofauti ya jamii kubwa ya Kiislamu ili kuweza kuzungumzia masuala yao mbalimbali ya kisiasa.
Hivi sasa pia kwa kuhuisha sura ya kisiasa ya Hija, kongamano hili adhimu la Kiislamu linaweza kutoa mchango mkubwa katika jiografia ya kisiasa ya dunia kwa kuleta mwamko, heshima na mshikamano wa umma wa Kiislamu. Mshikamano baina ya wananchi wa mataifa, ukifuatiwa na ule wa serikali katika Hija, ni bishara ya kudhihiri izza na nguvu za kidini; na kwa njia hiyo kuutangazia ulimwengu kuwa katika kulinda tunu na thamani zao za kidini, Waislamu watakabiliana na mchokozi yeyote dhidi ya ardhi za Kiislamu na fikra na itikadi za Waislamu. Hisham ibn Hakam amesema: "Nilimuuliza Imam Jaafar Sadiq (AS) kuhusu falsafa ya Hija na kutufu al-Kaaba; akasema:"Mwenyezi Mungu amewaumba waja wake hawa...akawapa amri mbalimbali zenye maslaha kwa dini na dunia, ikiwemo ya kujumuika watu wa mashariki na magharibi (katika ibada ya Hija), ili Waislamu waweze kujuana vizuri na kuelewana hali zao...na ili athari za Mtume SAW na habari zake zijulikane, watu wazikumbuke na wasije wakazisahau katu. Wassalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …