Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumamosi, 19 Septemba 2015 17:28

Dondoo za Hija (5)

Dondoo za Hija (5)

Hambambo wapenzi wasikilizaji na karibuni kutegea sikio makala hizi fupifupi zinazozungumzia fadhila za ibada ya hija, ambazo zinakujieni kwa mnasaba wa siku hizi adhimu za ibada hiyo ambayo ni moja ya nguzo muhimu za dini ya Kiislamu.
Hija ni ugeni wa Mwenyezi Mungu. Watu wanaokwenda hija na umrah wanahesabika kuwa wageni wa Mwenyezi Mungu, na ni kwa ajili hiyo ndio maana likawa jukumu la Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwakirimu wageni wake sanjari na kuwasamehe dhambi zao. Tazama kitabu cha Jaamiul-Hadith juzu ya 10 ukurasa wa 154. Wakati hujaji anapokuwa mgeni wa Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu, basi hukaribishwa na Muumba katika nyumba hiyo. Mwenyezi Mungu alimfunulia wahyi Nabii Adam (as) kwa kusema: "Mimi ni Mwenyezi Mungu mmiliki wa Makkah. Watu wa mji huo, miongoni mwa majirani na watu wenye kuuzuru mji huo, ni wageni wangu. Ninaufanya kuwa saada kwa ajili ya watu wa mbinguni na ardhini kundi kwa kundi waliochafuka kwa madhambi na wenye mavumbi, wote huja kufanya ziara kwenye al-Kaabah wakipiga takbira na kusema Labbaikallahumma labbaika!. Hivyo kila anayekusudia kufanya ziara na akawa hana nia nyingine ghairi ya hiyo, basi atakuwa amenizuru mimi na ni mgeni aliyekuja kwangu ambaye anastahiki kulipwa." Mwisho wa kunukuu. Ni suala lililo wazi kwamba ili kuhudhuria mbele ya Mola Mlezi na kushiriki katika ugeni wake, hujaji lazima ajiweke katika maadalizi mazuri, ambapo sanjari na kudhihirisha ikhlasi na ishqi ya hali ya juu ya kukutana na Mwenyezi Mungu, pia ajikurubishe kwake. Unapofika katika msikiti mtakatifu wa Makkah, basi tanguliza mguu wako uliopeku na unyenyekevu wa hali ya juu na kisha uingie. Wakati huo, mahujaji wanapodhihirisha utumwa wao mbele ya Mola wao, hupokelewa maombi yao yote kila pale watakapoomba dua. Wakiomba shufaa basi uombezi wao hupokelewa. Na hata kama watakaa kimya na wasiseme jambo, basi Mwenyezi Mungu huwalipa thawabu......Tazama kitabu cha Maladhul-Akhbar juzu ya 7 ukurasa wa 226.
Na kufikia hapa wapenzi wasikilizaji ninakuageni kwa kusema, Wassalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …