Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumamosi, 19 Septemba 2015 17:15

Dondoo za Hija (4)

Dondoo za Hija (4)

Assalaamu Alaykum wapenzi wasikilizaji na karibuni katika kipindi hiki kifupi kuhusu Hija. Leo tutaangazia Hija iliyokubaliwa au Haj maqbul. Haj Maqbul ni Hija ambayo hujidhihirisha pale mwanadamu anapojikomboa kutoka kujisifu na ubinafsi ambao huwa umemzunguka na kuficha ubora wa kipekee katika dhati ya nafsi yake.
Hija ni Fursa ya kipekee ambayo mbali na mtazamo wake wa kimaanawi na kiroho, pia huleta maingiliano mazuri baina ya mataifa ya Waislamu na hivyo izza na uwezo wa Waislamu ni sehemu ya baraka zake. Katika ibada hii yenye taadhima, maelfu ya wanadamu wakiwemo wanaume na wanawake waumini hutufu na kuswali kwa pamoja ambapo sawa na matone katika bahari isiyo na kikomo huwa wamezama katika rehma za Mwenyezi Mungu.
Pamoja na kuwepo tafauti zote baina yao, huwa wanapata tajiriba ya kuwa kitu kimoja kilicho imara huku wakijiimarisha na kuzidi kupata heshima. Hii inamaana kuwa, Hija si Ibada tu ambayo inajumuisha mwanadamu kutekeleza aina moja ya amali kavu zisizo na roho. Kama alivyosema Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kislamu, hatua moja ya mwanadamu kuelekea katika Mwenyezi Mungu hufanya moyo ujawe nana nuru na jampo hili humpa usindi. Hija huondoa kiza katika uono wa mwanadamu na hivyo kumsahilishia mkondo anaofuata.
Wakti moja mtu alirejea kutoka safari ya Hija na akaanza kumsimulia Imam Sadeq AS kuhusu safari hiyo na alioandamana nao. Alimsifu sana mmoja kati ya watu alioandamana nao katika safari kwa kusema: "Sisi tulikuwa na mtu mwenye hadhi na heshima. Katika kipindi chote alikuwa anajishughulisha na ibada tu na kila tulipofika katika nyumba alikuwa akienda katika katika kona maalumu na kusujudu huku akijishughulisha na ibada." Hapo Imam aliuliza "Basi ni nani aliyekuwa akifanya kazi zake, ni nani aliyekuwa akimshughulikia mnyama wake? Huyo bwana akajibu kwa kusema: Mini nlifanya kazi hiyo kwa fakhari naye alikuwa akijishughulisha na kazi takatifu tu na hivyo kazi kama mambo kama hayo hayakumshughulisha." Imam Akasema: "Kwa maelezo hayo wewe una hadhi ya juu zaidi yake"

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …