Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Alkhamisi, 17 Septemba 2015 19:52

Dondoo za Hija (3)

Dondoo za Hija (3)

Assalaamu alaykumu wapenzi wasikilizaji. Katika kipindi cha miaka kumi ya kuwa kwake mjini Madina, Mtume SAW hakuwa amehiji hadi pale iliposhuka aya ya 27 ya Surat al-Haj inayosema:
"Na watangazie watu Hija; watakujia kwa miguu na juu ya kila ngamia aliyekonda, wakija kutoka katika kila njia ya mbali."
Mtume SAW aliwaamrisha watoa wito na wenye kunadi wawatangazie watu wa Madina na viunga vyake kwa sauti ya wazi kwamba, mwaka huu Mtume SAW anataka kwenda Makka kwa ajili ya kutekeleza ibada ya Hija. Mamia ya Waislamu walikusanyika na wakaondoka pamoja naye kuekea Makka. Mtume SAW alikuwa kama kito cha thamani baina ya misafara ya Hija. Abdallah bin Rawahah alikuwa ameshika hatamu na zimamu ya kuongozea ngamia wa Mtume SAW na alikuwa akisoma mashairi kwa sauti ya wazi akisema:
Enyi watoto wa kufri na shirki mfungulieni Mtume njia na tambueni kwamba, yeye ni chemchemi na chimbuko la kheri na mambo mazuri."
Baada ya Mtume SAW kusikia mashairi hayo alimtaka Abdallah bin Rawahah badala ya kusoma mashairi hayo asome maneno haya, Laa ilaha illah Llah, Wahdahu Wahdahu Wahdah, Swadaqa Wa'adah, Nasara Abdahu, Wa'azza Jundahu" Ambayo tafsi yake ni
"Hapana Mola apasae kuabudiwa kwa hakia isipokuwa Mwenyezi Mungu, Yeye ni Mungu Mmoja, Yeye ni Mungu Mmoja, Yeye ni Mungu Mmoja, amesadikisha ahadi Yake, amenusuru mja Wake na amelipa izza na heshima jeshi lake."
Mtume SAW alikwenda miqati yaani maeneo ambayo watu wanapaswa kuvaa Vazi la Ihraam akiwa na wito wa umoja na mshikamano. Akaoga na kisha akavaa Vazi la Ihraam. Kisha akawa akiitikia wito wa Allah akisema: Labbayka na kutaja adhama na utukufu wa Mwenyezi Mungu. Wakati macho yake yalipoiona al-Kaaba, alinyanyua mikono yake juu na kupiga takbira na kisha akaomba dua kwa kusema:
"Ewe Mola, nakuomba kwa utukufu na adhama Yako, uzidishe haiba na wema wa nyumba hii na kila mtu ambaye atakuja kuhiji au kufanya Umra basi mzidishie utukufu, sharafu na wema wake." Kisha Mtume SAW akaelekea upande wa al-Kaaba na kugusa Hajar al-As'wad (Jiwe Jeusi) na baada ya hapo akajishughulisha na kufanya tawafu.
Katika safari hiyo Mtume SAW ambaye alikuwa mashuhuri kwa "Ukweli na Uaminifu" alikuwa akiwataka watu wasimamishe uadilifu na usawa, wasiseme uongo, wasichukue mali za wengine kwa dhulma, wasikanyage na kukiuka haki za wengine, wahurumiane, wadogo wawaheshimu wakubwa na wafanye juhudi za kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kwa dua, Swala na kufanya ibada.
Wassalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh....

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …