Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumanne, 15 Septemba 2015 17:08

Dondoo za Hija (1)

Dondoo za Hija (1)

Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh. Katika siku hizi wimbi bora zaidi ni lile ya sauti za Labbaika zinazotolewa na mahujaji wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu, al Kaaba wakijibu wito wa Nabii Ibrahim Khalilullah, na picha bora zaidi ni ile ya harakati inayokwenda kwa utulivu inayoshabihiana na mawimbi ya maji ya bahari ya mahujaji hao ambao licha ya kutofautiana katika rangi, lugha, mbari na makabila yao, wanazunguka Nyumba ya Mwenyezi Mungu kwa upendo, urafiki na kuhurumiana. Masjidul Haram ndio msikiti pekee wenye kumbukumbu ya twawafu na Swala za karibu Mitume elfu moja wa Mwenyezi Mungu na eneo pekee ambalo katika siku za Hija vigezo vyote vya kidhahiri huchanganyika, maskini na tajiri, mweusi na mweupe, mkuu na mdogo, mtawala na raia.. wote huwa katika safu moja na kutoa ujumbe wa kuwa waja wa Mwenyezi Mungu Mmoja kwa lugha ya mahaba na upendo, machozi ya ikhlasi na nyoyo zilizojaa shauku ya kukutana na Mola.
Hija ni miiraji na ngazi ya kuelekea katika maarifa na kumjua Mwenyezi Mungu, na mtu anayefaidika zaidi na ibada hiyo ni yule ambaye kabla ya kuhudhuria katika eneo lolote katika maeneo matakatifu, huwa amepiga hatua katika njia hiyo ya maarifa ya kumjua Allah SW. Imam Ali bin Abi Twalib (as) ambaye alikuwa mstari mbele katika kumjua Allah anasema katika Nahjul Balagha kwamba: Mwenyezi Mungu amekuwajibishieni Hija na kuifanya Batul Haram kuwa kibla cha watu na maelekeo ya wanaadamu wanaokwenda kwenye nyumba hiyo mithili ya njiwa wanaotafuta makimbilio ya amani. Mwenyezi Mungu ameijalia nyumba hiyo kuwa eneo la watu kudhihirisha uja na unyenyekevu wao mbele ya adhama yake...
Wassalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …