Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumamosi, 30 Aprili 2016 08:43

Madai ya serikali ya Msumbiji kuhusu usiri katika deni

Madai ya serikali ya Msumbiji kuhusu usiri katika deni

Waziri Mkuu wa Msumbiji amesema kuwa, machafuko nchini humo ndiyo sababu kuu iliyoifanya serikali kuamua kuficha habari kuhusu deni la dola bilioni moja na laki nne la nchi hiyo kwa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa IMF.

Carlos Agostinho do Rosário ameongeza kuwa, serikali ya Msimbiji imelazimika kuchukua mkopo huo kwa ajili ya kupambana na maharamia na kudhamini usalama wa meli za kibiashara katika fukwe za nchi hiyo. Tarehe 20 mwezi huu wa Aprili, Mfuko wa Fedha wa Kimataifa ulitangaza kuwa, utasimamisha misaada yake ya kifedha kwa Msumbiji kutokana na serikali ya nchi hiyo kutotimiza ahadi zake kwa shirika hilo. Antinette Sayeh mkurugenzi wa idara ya Afrika ya IMF amesisitiza kuwa, mfuko huo hautaipa serikali ya Msumbiji msaada wowote wa kifedha hadi itakapolipa deni la dola bilioni moja kwa chombo hicho. Wiki chache zilizopita, Mfuko wa Fedha wa Kimataifa ulikataa kutuma wataalamu wake mjini Maputo ambao walitarajiwa kuipa serikali ya Msumbiji msaada wa dola milioni 283. Mwezi Disemba mwaka 2015 IMF iliipa serikali ya Msumbiji msaada wa dola milioni 117. Kabla ya hapo pia yaani mwezi Disemba 2014, Mfuko wa Fedha wa Kimataifa ulikata misaada yake kwa nchi maskini ya Mali baada ya viongozi wa nchi hiyo kuamua kunua ndege ya rais kwa gharama ya dola bilioni 40 badala ya kutumia fedha hizo katika miradi ya maendeleo. Misaada ya IMF kwa nchi za Afrika inatolewa kwa shabaha ya kuzisaidia nchi hizo kupambana na migogoro ya chakula. Msumbiji iliyoko kusini mashariki mwa Afrika, ina watu milioni 24 na inahesabiwa kuwa moja ya nchi maskini zaidi duniani. Ukame wa mara kwa mara na mafuriko yanayotokana na hali mbaya ya hewa ni katika mambo ambayo yanazifanya nchi za Msumbiji na Malawi kuhitajia misaada ya daima ya kibinadamu. Hivi karibuni serikali ya Maputo iliomba msaada wa dola milioni 180 kutoka kwa IMF kwa ajili ya kukabiliana na kukabiliana na matatizo yake mbalimbali. Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa Msumbiji amekwenda Washington Marekani kwa ajili ya kuonana na viongozi wa IMF baada ya shirika hilo kukata misaada yake kwa Msumbiji. Wakati huo huo tarehe 23 Aprili serikali ya Msumbiji ilikiri kuwa inadaiwa dola bilioni moja na laki nne na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa. Serikali hiyo ilikuwa inakanusha kuwa na deni hilo hadi IMF ilipoamua kusimamisha misaada yake. Hatua ya Waziri Mkuu wa Msumbiji ya kukiri kuweko ukosefu wa usalama nchini humo ni katika kuashiria mgogoro wa kisiasa uliopo baina ya waasi wa zamani wa Renamo na serikali ya hivi sasa ya nchi hiyo. Chama cha Renamo ambacho sasa ni cha kisiasa, hadi leo hii kinaendelea kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2014 suala ambalo limeendelea kuleta hali ya wasiwasi nchini humo hususan katika maeneo ya katikati na kaskazini mwa Msumbiji. Machafuko baina ya wafuasi wa chama cha Renamo na askari wa serikali yaliongezeka mwezi Februari mwaka huu. Wachambuzi wa mambo wanaamini kuwa, hatua ya baadhi ya viongozi wa nchi za Afrika ya kung'ang'ania madaraka, kitendo cha vyama tawala kutafuta kila njia za kuhakikisha having'olewi madarakani na ufisadi mkubwa serikalini ni katika matatizo sugu barani Afrika. Fauka ya hayo, wananchi wa Msumbiji walipata matumaini ya kupungua matatizo yao baada ya kugunduliwa akiba ya mafuta nchini mwao, lakini kuporomoka vibaya bei ya mafuta katika soko la dunia kumewakatisha tamaa wananchi hao hasa baada ya thamani ya sarafu ya Msumbiji kuporoka kwa asilimia 30 mbele ya dola ya Kimarekani.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …