Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Ijumaa, 29 Aprili 2016 19:32

Wajibu wa Marekani kuilipa fidia Iran

Wajibu wa Marekani kuilipa fidia Iran
Waziri wa Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amemtaka Karibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aishinikize serikali ya Marekani iheshimu makubaliano ya kimataifa na iilipe fidia Iran.

Jana Alkhamisi, Muhammad Javad Zarif alilalamikia hatua ya Mahakama Kuu ya Marekani ya kuzuia kulipwa karibu dola bilioni mbili za mali za Iran kupitia barua aliyomwandikia Ban Ki moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na kumtaka aishinikize serikali ya Marekani iheshimu sheria za kimsingi za kulinda haki za nchi nyingine na kuyapiga marufuku mabenki ya Marekani kuzuia mali za Iran. Vile vile amemtaka Ban Ki moon aishinikize serikali ya Marekani iheshimu makubaliano ya kimataifa na iache kuweka vizuizi katika miamala ya kifedha na kibiashara ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na nchi za nje kama yanavyosema makubaliano ya nyuklia ya JCPOA. Zarif amesema, serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina haki ya kuchukuwa hatua zinazotakiwa kwa ajili ya kurejesha haki na kulinda manufaa ya wananchi wa Iran mbele ya vitendo vilivyo kinyume na sheria vinavyoendelea kufanywa na Marekani. Tarehe 20 mwezi huu wa Aprili, Mahakama Kuu ya Marekani ilichukua hatua iliyo kinyume na sheria za kimataifa ya kupasisha kuwa mahakama za Marekani zinaweza - kupitia mashtaka ya wahanga wa makosa eti ya kigaidi - kuzuia mali za Iran kama njia ya kuwalipa fidia wahanga hao. Marekani inadai kuwa eti Iran ilihusika katika mripuko wa wanajeshi wa Marekani mjini Beirut Lebanon mwaka 1983. Vile vile mahakama moja mjini New York hivi karibuni imedai kuwa eti mashambulio ya kigaidi ya tarehe 11 Septemba mwaka 2001 nchini Marekani amri yake ilitokea nchini Iran ili kwa kupitia madai ya mahakama hiyo ya New York, Marekani iweze kuzuia dola bilioni kumi na nusu za mali ya Iran na kuwapa wahanga wa mashambulio hayo ya kigaidi. Ni jambo lililo wazi kuwa hatua kama hizo za vyombo vya mahakama vya Marekani zinazidi kuvipotezea itibari vyombo hivyo vya Marekani. Kwa hakika ni Marekani ndiyo inayopaswa kuilipa fidia Iran kutokana na uadui na jinai zake kubwa dhidi ya taifa hili. Maarekani inaihusisha Iran na mambo ambayo haikufaya katika hali ambayo Tehran iko mstari wa mbele katika vita vya kimataifa vya kupambana na ugaidi. Madai kuwa Iran eti ilihusika kwenye mashambulio ya Septemba 11 ya nchini Marekani ni kichekesho kikubwa mno na kichungu ambacho kinaonesha namna mahakama ya Marekani inavyohalalisha mashambulio hayo kwa kuwatoa hatiani wahusika halisi wa ugaidi huo. Kurasa 28 za ripoti ya mashambulio ya Septemba 11, 2001 zinazoonesha kuwa Saudi Arabia ilihusika moja kwa moja kwenye mashambulio hayo ya kigaidi zimefichwa na hilo linaonesha namna Washington ilivyo tayari kulinda uhusiano wake na Riyadh kwa thamani yoyote ile. Kwa kweli kutumiwa madai ya ugaidi kwa ajili ya kuzuia mali na fedha za Iran hakutokani na kitu kingine ghairi ya uadui wa kila siku wa Marekani dhidi ya wananchi wa Iran. Siasa za kiuadui za Marekani dhidi ya taifa la Iran na madhara waliyopata wananchi wa Iran kutokana na siasa hizo za Marekani ni mambo ambayo yana ushahidi makini wa kihistoria. Moja ya mfululizo wa vitendo vya kiadui vya Marekani dhidi ya Iran ni mapinduzi ya tarehe 19 Agosti 1953 yaliyofanywa na Wamarekani dhidi ya serikali halali iliyochaguliwa na wananchi wa Iran. Mifano mingine ya wazi ni misaada ya kijasusi na misaada mengine mbalimbali ya Marekani kwa utawala wa Kibaath wa Saddam katika vita vilivyoanzishwa na utawala wa wakati huo wa iraq dhidi ya Iran. Mfano mwingine ni namna Wamarekani ulivyousaidia utawala wa Saddam kutumia silaha za kemikali dhidi ya wanajeshi na raia wa Iran, masuala ambayo ni jinai za wazi za kivita. Mfano mwingine ni jinai ya wanajeshi wa Marekani ya kutungua ndege ya abiria ya Iran ikiwa na wasafiri 290. Na hiyo ni mifano michache mno ya jinai za Marekani dhidi ya wananchi wa Iran ambazo zina ushahidi madhubuti ambao uko pia mikononi mwa Umoja wa Mataifa. Ushahidi huo kwa hakika unasafisha njia ya kuweza taifa la Iran kuishitaka Marekani na kuilazimisha kulilipa fidia taifa hili.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …