Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Ijumaa, 29 Aprili 2016 11:30

Wasiwasi kuhusu hali ya mambo nchini Algeria

Wasiwasi kuhusu hali ya mambo nchini Algeria
Ali Benflis, Waziri Mkuu wa zamani wa Algeria alisema siku ya Jumatano kwamba hali ya kisiasa na kiuchumi ya nchi hiyo inatia wasiwasi.

Benflis ambaye ni mmoja wa wapinzai wakuu wa serikali anasema kuwa hali hiyo inatokana na kushindwa serikali kutekeleza majukumu yake na kwamba inaonyesha kuwa Rais Abdelaziz Bouteflika wa nchi hiyo hana tena uwezo wa kuongoza nchi. Kuchapishwa picha ya Bouteflika katika gazeti la Ufaransa la Le Monde na kutuhumiwa kwake kukwepa kulipa kodi katika faili la kasha ambayo imekuja kujilikana kama Karatasi za Panama, kashafa ambayo inatajwa kuwa Watergate ya karne, kumezidi kuiweka pabaya serikali ya Algeria na kuifanya ikabiliwe na changamoto chungu nzima. Jambo hilo pia limezua mvutano kati ya serikali ya Algeria na Ufaransa. Rais Bouteflika alitwaa uongozi wa Algeria mwaka 1999 ambapo alipata fursa ya kuendelea kuongoza nchi hiyo kupitia uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka 2004. Lakini kama walivyo viongozi wengine wengi wakongwe walio na kiu kali ya madaraka barani Afrika, Bouteflika alibadili katiba ya Algeria na hivyo kujipa fursa ya kuendelea kuitawala nchi hiyo. Kufikia sasa Bouteflika amebadili katiba ya nchi hiyo mara mbili bila kufanyika kura ya maoni. Kwa msingi huo alichaguliwa kwa mara ya tatu mwaka 2009 na kwa mara ya nne mwaka 2014 kuwa rais wa Algeria bila kuwepo upinzani wowote wa maana dhidi yake. Hata hivyo kushiriki kwake kwa mara ya nne katika uchaguzi mkuu kuliwakasirisha sana Walgeria na kupelekea kuzuka machafuko nchini humo. Mbali na kulalamikia hali mbaya ya uchumi wa Algeria wananchi wa nchi hiyo pia wamekuwa wakilalamikia hali isiyoridhisha ya kisiasa ambayo imekuwa ikitawala katika nchi hiyo katika miaka ya hivi karibuni. Hivi sasa kashfa ya Karatasi za Panama dhidi ya Rais Bouteflika imewapa wapinzani wake fursa nzuri ya kutoa mashinikizo dhidi yake na kutaka uongozi wa nchi hiyo ubadiishwe. Kashfa hiyo inayotajwa kuwa kubwa zaidi kuwahi kufichuliwa na vyombo vya habari tayari imewahusisha viongozi 12 wa nchi mbalimbali za dunia na pia wanasiasa mashuhuri 72. Kwa muda wa karibu mwaka mmoja, maripota wa mashirika muhimu ya habari duniani walishirikiana kwa karibu na hatimaye kufichua kashfa hiyo mwanzoni mwa mwaka huu. Uchunguzi huo wa wanahabari uliweza kuweka wazi namna watu wachache walio na madaraka na uwezo wa kifedha na ambao huhisi kwamba hawawajibiki mbele ya mtu yoyote yule, wanavyotumia njia zisizo za kisheria kuficha na kujirundikia utajiri mkubwa nje ya nchi zao. Kuhusu faili hilo la Karatasi za Panama shirika la Mossack Fonseca, ambalo kwa hakika ni shirika linalojishughulisha na masuala ya kisheria kuhusu biashara ya kimataifa, limetuhumiwa kubadilika na kuwa sehemu salama ya wanasiasa na wafanyabiashara mashuhuri wa kimataifa kufanyia uhalifu wa ukoshaji fedha chafu. Wataalamu wa mambo wanaamini kwamba kashfa ya Panama bila shaka itachochea ghasia na machafuko ya kisiasa katika nchi tofauti za dunia ikiwemo Algeria, na kwamba kuna uwezekano wa machafuko hayo kusababisha maafa katika nchi hizo. Hii ni kwa sababu kashfa hiyo ni tishio kwa tawala za kibeberu na bila shaka serikali zilizohusishwa na kashfa hiyo zitatumia kila njia ili kutetea nafasi yazo kitaifa na kimataifa.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …