Chapisha ukurasa huu
Ijumaa, 29 Aprili 2016 08:37

Mwangwi wa mgogoro wa kibinadamu katika Ukanda wa Gaza

Mwangwi wa mgogoro wa kibinadamu katika Ukanda wa Gaza
Ripoti mbalimbali kutoka Ukanda wa Gaza huko Palestina zinasema kuwa, hali ya mambo katika eneo hilo imezidisha wasiwasi wa fikra za waliowengi duniani na inaakisi mgogoro mkubwa wa kibinadamu katika eneo hilo linalozingirwa na Wazayuni maghasibu.

Kufuatia hali hiyo jamii ya kimataifa na asasi na mashirika ya kimataifa ya misaada ya kibinadamu yametahadharisha kuhusu uwezekano wa kuendelea hali hiyo na vizingiti vinavyowekwa na Israel katika njia hiyo na kusisitzia kuwa, hali mbaya na ya maafa ya Gaza inatishia maisha ya wakazi zaidi ya milioni moja na nusu wa eneo hilo la Palestina.

Katika upande mwingine Israel inaendelea kuzuia shughuli za jumuiya na mashirika ya misaada ya kibinadamu katika eneo hilo linalozingirwa. Isam Yusuf ambaye ni mratibu wa masuala ya misafara inayotoa misaada ya kibinadamu kwa watu wa Gaza amesema kuwa jeshi la Israel linawakamata na kuwasali wafanyakazi wa taasisi za kimataifa na limefuta vibali vya wanadiplomasia kuingia katika Ukanda wa Gaza kwa shabaha ya kuzidisha mzingiro wa eneo hilo.

Utawala haramu wa Israel unalizingira eneo la Ukanda wa Gaza kwa karibu muongo mmoja sasa na unazuia kuingizwa zana na bidhaa muhimu kama nishati, chakula na dawa katika eneo hilo lenye jamii kubwa ya watu. Suala hilo limezidisha hali mbaya ya raia wa Gaza na kupiga kengele ya hatari kuhusu uwezekano wa kutokea maafa ya kibinadamu. Mzingiro huo wa Israel umewafanya watu wa Gaza wakose huduma na bidhaa muhimu kama maji, dawa, mavazi na chakula. Sambamba na hayo jeshi la Israel limekuwa likifanya mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya wakazi wa Ukanda wa Gaza na kukiuka makubaliano ya kusitisha vita kati ya pande mbili. Makubaliano hayo yalifikiwa Agosti mwaka 2014 baada ya mashambulizi makali ya siku 50 ya jeshi la utawala huo ghasibu dhidi ya raia wasio na hatia wa Palestina. Zaidi ya raia 2300 wa Palestina waliuawa shahidi katika mashambulizi hayo na maelfu ya wengine walijeruhiwa. Israel pia iliharibu kikamilifu miundombinu ya eneo hilo na inazuia juhudi za kimataifa za kulikarabati na kulijenga upya eneo hilo.

Wakati ho huo uzembe wa jamii ya kimataifa hususan Umoja wa Mataifa na kutokabiliana ipasavyo na utawala huo haramu vimeipa Israel fursa ya kuzidisha uhalifu na jinai zake dhidi ya watu wa Palestina.

Kwa ujumla tunaweza kusema kuwa, mwenendo wa Umoja wa Mataifa katika kadhia ya Palestina umekuwa kana kwamba hakuna maafa wala mgogoro mkubwa wa kibinadamu katika eneo la Ukanda wa Gaza. Kupuuzwa hali mbaya na maafa ya Gaza katika mkutano wa kila mwaka wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ni mfano wa wazi wa mwenendo huo usio wa kuwajibika wa jamii ya kimataifa hususan Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya Palestina.

Maandiko yanayofanana

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)