Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Alkhamisi, 28 Aprili 2016 08:11

Baraza la Usalama UN lapinga ubeberu wa Israel

Baraza la Usalama UN lapinga ubeberu wa Israel

Katika kuendelea upinzani wa kimataifa dhidi ya hatua za kichokozi na ukaliaji ardhi za nchi nyingine unaofanywa na utawala haramu wa Israel huko katika eneo la Golan nchini Syria, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa mara nyingine tena limetaka kuondoka mara moja askari wa utawala huo ghasibu katika eneo hilo.

Kuhusu suala hilo Liu Jieyi, mwakilishi wa Uchina katika Umoja wa Mataifa na ambaye nchi yake ni mwenyekiti wa hivi sasa wa Baraza la Usalama alisema siku ya Jumanne kwamba wanachama 15 wa Baraza hilo wameelezea wasiwasi wao mkubwa kuhusiana na matamshi ya kichochezi yaliyotolewa hivi karibuni na waziri mkuu wa utawala haramu wa Israel kuhusiana na miinuko ya Golan na kusisitiza kuwa hali ya miinuko hiyo haitafanyiwa mabadiliko yoyote. Mwakilishi huyo wa Uchina amesema kwa mujibu wa azimio nambari 497 la Umoja wa Mataifa ambalo lilipitishwa mwaka 1981, hatua ya Israel ya kujaribu kutekeleza sheria za kiidara katika eneo hilo la Golan ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa. Katika kikao kisicho cha kawaida cha baraza la mawaziri la utawala ghasibu wa Israel ambacho kilifanyika katikati ya mwezi huu huko katika miinuko hiyo ya Golan, Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala huo alisema kuwa miinuko hiyo itaendelea kuwa chini ya udhibiti wa utawala huo milele. Radiamali ya kimataifa na hasa ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika mazingira ya hivi sasa inathibitisha wazi kwamba jamii ya kimataifa kamwe haitakubali siasa za kujitanua na za kibeberu za utawala huo wa Kizayuni. Pamoja na hayo utawala huo ghasibu ambao katu hauheshimu sheria za kimataifa, unatumia mbinu tofauti kuendelea kujiimarisha katika ardhi za Waarabu unazozikalia kwa mabavu ikiwemo miinuko ya Golan nchini Syria kwa kujaribu kubadilisha miundo ya kijamii na mifumo ya kijografia katika ardhi hizo. Kuongezeka kwa fitina na njama za utawala huo dhidi ya serikali ya Syria kunabainisha wazi tamaa ya utawala huo kwa taifa la Syria, suala ambalo linaonyesha wazi kwamba utawala huo na waungaji mkono wake wakuu na hasa Marekani ndio wanachochea mgogoro wa hivi sasa wa nchi hiyo kupitia makundi ya kigaidi na kitakfiri. Utawala wa kibaguzi wa Israel unatumia mbinu tofauti kulazimisha jamii ya kimataifa ikubali siasa zake za kujitanua Mashariki ya Kati lakini kufuatia azimio lake la hivi karibuni, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limethibitisha wazi kwamba jamii ya kimataifa haiko tayari kukubali jambo hilo. Ni nyema tukumbushe hapa kuwa maazimio mengine ya Baraza la Usalama yakiwemo ya 242 na 338 pia yanautaka utawala huo uondoke mara moja katika ardhi unazozikalia kwa mabavu huko Palestina, Lebanon na Syria. Lakini utawala huo kwa kutegemea uungaji mkono mkubwa unaopata kutoka kwa madola makubwa duniani na hasa Marekani umekuwa ukiendelea na siasa zake za ubabe na kujitanua katika eneo bila kuhofia lolote. Pamoja na hayo yote lakini matukio ya hivi sasa kimataifa yanathibitisha wazi kwamba jamii ya kimataifa sasa iko dhidi ya siasa hizo za utawala haramu wa Israel na inaelekea kuunga mkono haki za kimsingi za taifa la Palestina. Kulaaniwa mara kwa mara utawala haramu wa Israel na Umoja wa Mataifa bila shaka kuna mchango mkubwa katika kuwafahamisha walimwengu utambulisho halisi wa kigaidi na kibaguzi wa utawala huo. Hata hivyo kutosheka tu Baraza la Usalama na kuulaani kwa maneneo matupu utawala huo hakutasaidia pakubwa katika kuufanya usitishe siasa zake hizo katika ardhi za mataifa ya Kiarabu na Kiislamu, kama tunavyoshuhudia ukweli huo mchungu katika matukio ya huko nyuma. Tabia hiyo ya Baraza la Usalam inathibitisha wazi upendeleo wake kwa utawala huo unaoendelea kufanya jinai na uharibifu mkubwa katika ardhi unazozikalia kwa mabavu. Tabia hiyo bila shaka imeufanya utawala huo uzidi kumea pembe na hivyo kuufanya udumishe siasa zake za kibeberu na kujitanua katika eneo.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …