Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatano, 27 Aprili 2016 12:25

Machafuko ya Burundi yaitia wasiwasi jamii ya kimataifa

Machafuko ya Burundi yaitia wasiwasi jamii ya kimataifa
Machafuko yanayoendelea kushuhudiwa katika nchi ya Burundi yameitumbukiza nchi hiyo katika mgogoro mkubwa. Mauaji ya Waziri wa Haki za Binadamu, Martin Nivyabandi na mkewe na yale ya hivi majuzi ya Athanase Kararuza aliyekuwa mshauri wa masuala ya kijeshi wa Rais wa Burundi, yameizamisha zaidi nchini hiyo katika lindi kubwa la machafuko na ukosefu wa amani.

Baada ya mauaji hayo, Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi alisema watekelezaji wa mauaji hayo wanapaswa kutiwa nguvuni haraka iwezekanavyo na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria. Hata hivyo wakosoaji wanasema Rais Nkurunziza mwenyewe amechangia pakubwa katika hali ya sasa ya Burundi.

Burundi ilitumbukia katika machafuko ya ndani Aprili mwaka jana baada ya chama tawala cha CNDD-FDD kumuidhinisha Rais Mkurunziza kuwania tena kiti hicho kwa mara ya tatu mfululizo. Hadi sasa zaidi ya watu 400 wameuawa katika machafuko hayo na zaidi ya laki mbili na nusu kukimbilia katika nchi jirani kama Tanzania, Rwanda na Congo DR.

Mauaji na machafuko mapya ya Burundi yameitia wasiwasi mkubwa jamii ya kimataifa. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa taarifa akilaani mauaji ya Athanase Kararuza na kutoa wito wa kufanyika uchunguzi kamili kuhusu mauaji hayo.

Wakati huo huo Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) Bi Fatou Bensouda ametangaza kwamba, amefungua fali la kuchunguza hali ya Burundi. Bensouda amesema amewatahadharisha viongozi wa Burundi juu ya uwezekano wa kufanyika jinai katika nchi hiyo na kwamba mahakama yake itafuatilia uhalifu huo.

Kwa sasa watu wa Burundi wanasumbuliwa na mapigano ya kila siku, kuhama makundi ya watu, majaribio ya mapinduzi, mauaji ya wanasiasa na viongozi wa jeshi kutokana na kiu ya madaraka isiyokatika ya Rais Pierre Nkurunzinza.

Kinyume na hali ya nchi jirani ya Rwanda baada ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 ambapo vigezo vyote vya ukabilia vilitupiliwa mbali na kufutwa, Katiba ya Burundi imeainisha hisa ya fungu la watu wa kabila la Watutsi, sehemu ya kabila la Wahutu na ile ya Watwa katika Bunge la nchi hiyo. Vilevile makubaliano ya amani ya Arusha kati ya makundi hasimu ya Burundi yanasisitiza suala la kuwepo sehemu ya kila kabila katika jeshi, taasisi na idara za serikali. Pamoja na hayo wakosoaji wanasema Rais Nkurunziza amepuuza hata vipengee hivyo vya katiba na makubaliano ya Arusha.

Kwa kutilia maanani hali ya sasa ya Burundi wadadisi wa mambo wanasema kuwa, kuendelea kwa hali ya sasa kutaitumbukiza Burundi katika hali mbaya zaidi na kutishia usalama wa kanda nzima ya Maziwa Makuu ya Afrika.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …