Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatano, 27 Aprili 2016 07:03

Malalamiko ya chama tawala nchini Afrika Kusini dhidi ya matamshi ya wapinzani

Malalamiko ya chama tawala nchini Afrika Kusini dhidi ya matamshi ya wapinzani
Chama tawala nchini Afrika Kusini kimetoa taarifa na kutangaza kuwa, matamshi ya Julius Malema mmoja wa wapinzani wa Rais Jacob Zuma ni hiana na usaliti dhidi ya maslahi ya kitaifa na kwamba, serikali ya nchi hiyo itamshtaki.

Julius Malema kiongozi wa upinzani nchini Afrika Kusini ametishia kwamba, ili kuiondoa madarakani serikali ya Zuma yuko tayari kutumia nguvu na hata ikibidi atabeba silaha. Malema ambaye ni mkuu wa chama cha Economic Freedom Fighters anamtuhumu Rais Zuma kwa ubadhirifu na anataka kiongozi huyo auzuliwe madarakani.

Hata kama baadhi ya wajumbe wa chama tawala cha ANC na shakhsia wengine wamemtaka Rais Zuma aachie ngazi, lakini inasemekana kwamba, chama hicho kinamuunga mkono Bwana Zuma.

Hata hoja ya kutaka kumpigia Rais Zuma kura ya kutokuwa na imani naye iliowasilishwa bungeni na wapinzani iligonga mwamba kutokana na kutopata kura zinazohitajika. Wabunge 233 walipinga hoja hiyo huku 143 wakiunga mkono na kwa utaratibu huo Rais Zuma akanusurika na kura ya kutokuwa na imani naye.

Julius Malema anayehesabiwa kuwa mmoja wa wapinzani wakuu wa Rais Jacob Zuma amedai kwamba, viongozi wa baadhi ya vyama vya upinzani nchini Afrika Kusini kwa uongozi wake wameahidi kwamba, hawataacha mpango wao wa kutaka kung'olewa madarakani Rais Zuma. Rais wa Afrika Kusini anaungwa mkono na jumuiya za wanawake za chama tawala cha ANC, majeruhi wa vita , waliopambana dhidi ya utawala wa zamani wa ubaguzi wa rangi na wanaharakati wa zamani wa kisiasa wa chama tawala. Aidha Zuma anaungwa mkono na Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi nchini humo.

Baadhi ya weledi wa mambo wanaamini kwamba, himaya kubwa ya vyama na matawi ya jumuiya za wanawake za ANC ndiyo nguvu na kiegemeo cha Rais Zuma kuendelea kuweko madarakani.

Tuhuma za kutumia fedha za serikali kwa ajili ya kukarabati makazi yake binafsi ni kashfa ambayo ingeweza kumuondoa madarakani Rais yeyote yule. Lakini viongozi wa chama tawala cha ANC ambao ni wanaharakati wenzake wakati wa mapambano dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini walizuia kwa wakati unaofaa kushughulikiwa faili la Zuma la kutumia vibaya fedha za umma.

Katika mazingira kama haya, Julius Malema, kiongozi wa zamani wa tawi la vijana la ANC anasema kuwa, atafichua mambo ambayo yataandaa uwanja wa kuondolewa madarakani Rais Zuma. Rais Zuma alishika usukuni wa kuiongozi Afrika Kusini kwa duru ya pili mwaka 2014 baada ya kuwashinda wapinzani wake. Pamoja na hayo hatupaswi kusahau nafasi athirifu ya mzee Nelson Mandela katika kushinda Zuma zoezi la uchaguzi huo.

Mandela ambaye anajulikana kuwa nembo ya vita dhidi ya ubaguzi wa rangi aliaga dunia Disemba 5 mwaka 2013. Kabla ya kufariki kwake dunia hakusita hata kidogo kuunga mkono kupitishwa Zuma kugombea tena Urais kwa tiketi ya chama tawala cha ANC.

Vyama vya upinzani kama Democratic Alliance (DA) kwa muda sasa vimekuwa vikitaka chama tawala cha ANC kiondolewe madarakani. Filihali, Julius Malema mkuu wa chama cha Economic Freedom Fighters na Helen Zille kiongozi wa zamani wa chama cha Democratic Alliance (DA) wameungana na kuwa na sauti moja.

Kwa sasa kwa kuzingatia kwamba, hakuna muungaji mkono mwenye kuheshimiwa kama alivyokuwa mzee Nelson Mandela, bila shaka Rais Jacob Zuma anakabiliwa na mpambano mkali kutoka kwa wapinzani.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …