Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumanne, 26 Aprili 2016 17:14

Sisitizo la Iran na Russia juu ya kuupa kipaumbele mkakati wa kupambana na ugaidi

Sisitizo la Iran na Russia juu ya kuupa kipaumbele mkakati wa kupambana na ugaidi
Jumanne ya leo tarehe 26 Aprili, Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kislamu ya Iran ameelekea katika mji mkuu wa Russia Moscow akiuongoza ujumbe wa ngazi za juu wa nchi yake.

Brigedia Jenerali Hussein Dehqan ameelekea Russia kwa mwaliko wa Sergey Kuzhgetovich Shoygu Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo kwa ajili ya kwenda kushiriki katika kongamano la kila mwaka la kimataifa la usalama. Akiwa nchini humo, Brigedia Jenerali Dehqan atakutana na kufanya mazungumzo pia na baadhi ya viongozi wa ngazi za juu wa nchi hiyo kuhusiana na suala la kustawisha uhusiano wa kiulinzi.

Kongamano la tano la kimataifa la usalama linatarajiwa kufanyika kwa muda wa siku mbili kuanzia kesho huko Moscow huku ajenda kuu likiwa ni suala la kupambana na ugaidi. Shakhsia 500 wakiwemo mawaziri 17 wa ulinzi na manaibu waziri wa ulinzi 14 wanatarajiwa kushiriki katika kongamano hilo.

Katika kongamano hilo, washiriki wanatarajiwa kujadili mkakati wa kupambana na ugaidi pamoja na kuunganisha mitazamo ya kimataifa katika kukabiliana na tatizo hilo. Aidha masuala ya usalama wa eneo la Asia na Bahari ya Pacific, uthabiti wa kimataifa na ushirikiano wa kijeshi nayo ni mambo yanayotarajiwa kujadiliwa katika kongamano hilo la siku mbili.

Iran na Russia zinasisitiza juu ya kuweko mkakati wa pamoja wa kupambana na ugaidi na uratibu uliojitokeza umeweza kuzuia kusonga mbele tishio na hatari ya ugaidi katika Mashariki ya Kati. Katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita Waziri wa Ulinzi wa Iran amefanya safari mbili mbili nchini Russia.

Duru kadhaa za mazungumzo ya Mawaziri wa Ulinzi wa Iran na Russia, safari ya Brigedia Jenerali Dehqan huko Moscow mwezi Januari mwaka huu na kisha mazungumzo yake na Rais Vladimir Putin na vilevile safari ya Waziri wa Ulinzi wa Russia hapa Tehran kwa ajili ya kufuatilia mazungumzo ni mambo yanayoonesha kuendelea kuweko mitazamo ya pamoja ya nchi mbili hizi kuhusiana na masuala ya Mashariki ya Kati.

Safari ya sasa ya Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Russia na kushiriki ujumbe wa Iran katika kikao cha kimataifa cha usalama mjini Moscow ambacho ajenda yake kuu ni vita dhidi ya ugaidi ni ishara ya kupiga hatua mitazamo ya pamoja ya Moscow na Tehran katika uga wa kieneo.

Kuongezeka ushirikiano wa kieneo wa Iran na Russia ni natija ya uhusiano mzuri wa kisiasa wa pande mbili na bila shaka sisitizo la viongozi wa nchi mbili la kupanuliwa zaidi ushirikiano imekuwa chachu ya kuendelea kuweko misimamo ya pamoja katika masuala ya kieneo zikiwemo juhudi za kuipatia ufumbuzi migogoro wa Syria, Iraq na Yemen na vile vile kuundwa muungano mpana wa kimataifa wa kupambana na ugaidi.

Katika fremu ya ushirikiano wa kiisteratejia, Marais Hassan Rouhani wa Iran na Vladimir Putin wa Russia wameshakutana mara saba hadi sasa na mara ya mwisho walikutana Novemba mwaka jana hapa mjini Tehran.

Wachambuzi wa mambo wanaamini kuwa, mazungumzo katika kiwango cha Marais na viongozi wengine wa nchi mbili hizo yamepelekea kuongezeka mitazamo ya pamoja katika matukio ya Mashariki ya Kati hususan kadhia ya mgogoro wa Syria.

Ukweli ulio wazi ni kwamba, Iran na Russia zinalipa kipaumbele katika siasa zao za kigeni suala la kupambana na ugaidi na misimamo ya kuchupa mipaka na zimeweza katika uwanja huo kuifanya jamii ya kimataifa izingatie suala la kupambana kwa dhati na masuala hayo.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …