Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumanne, 26 Aprili 2016 09:19

Saudi Arabia yazidi kukumbwa na matatizo ya kiusalama na kiuchumi

Saudi Arabia yazidi kukumbwa na matatizo ya kiusalama na kiuchumi

Nakisi kubwa na isiyo na kifani ya bajeti ya Saudi Arabia kutokana na uingiliaji kijeshi ufalme huo katia nchi jirani ya Yemen na pia kujiingiza katika masuala ya ndani ya nchi za eneo ni mambo ambayo yamepelekea watawala wa ukoo wa Aal Saud kujipata katika hali ngumu.

Siku chache zilizopita, baada ya kuchapishwa ripoti ya Mfuko wa Uwekezaji Saudia kuhusu nakisi ya bajeti ya makumbi ya mabilioni ya dola, Mfuko wa Kimataifa wa Fedha IMF umetangaza kuwa Saudia inakumbwa na nakisi ya dola bilioni 140 katika bajeti yake na kuongeza kuwa, nchi hiyo haina budi ila kutafuta njia za kukabiliana na tatizo hilo.

Mfumo wa Uwekezaji Saudia umetoa taarifa na kusema, kwa mujibu wa amri za watawala wa nchi hiyo, ili kukabiliana na changamoto iliyopo ya kiuchumi, mfuko huo umeshurutishwa kuwaajiri wataalamu bora zaidi wa benki na uchumi duniani ili kuitafutia Saudia njia ya kujiondoa katika tatizo kubwa la kiuchumi inalokabiliana nalo.

Mohammad bin Salman, mwana wa Mfalme Salman wa Saudia, ambaye mbali na kuwa naibu mrithi wa kiti cha ufalme, pia ni waziri wa ulinzi nchini humo, amesema kutokana na ongezeko la matumizi ya kijeshi na changamoto za kiusalama, Saudia sasa inakumbwa na matatizo ya kiuchumi. Amesema ili kujikwamua kutoka hali hiyo, kuna mipango kadhaa itakayotekelezwa na mojawapo ni kuuza hisa za shirika kubwa la mafuta nchini humo Aramco.

Siku kadaa zilizopita pia, Mohammad Aal Sheikh, mshauri wa ngazi za juu wa Mohammad bin Salman alisema, iwapo nchi hiyo haitatafakari njia za kutatua matatizo yake ya kiuchumi katika kipindi cha miezi michache ijayo, basi itafilisika kikamilifu ifikapo mwaka 2017.

Duru ndani za Saudia zinadokeza kuwa Naibu Mrithi wa Kiti cha Ufalme Mohammad bin Salman amewasilisha mpango wa dharura wa kuunusuru ufalme huo kutokana na hali mbaya ya kiuchumi iliyofanywa mbaya zaidi na hujuma ya kijeshi Yemen.

Mpango huo umewasilishwa katika hali ambayo Jumamosi Mfalme Salman alimfuta kazi Waziri wa Maji na Umeme Abdullah Al-Hussayen. Waziri huyo amefutwa kazi kama njia ya kutuliza hasira za wananchi kufuatia kuongozeka kwa kiwango kikubwa cha bei ya maji na umeme nchini humo. Tokea Mfalme Salman aingie madarakani mwaka mmoja na nusu uliopita amewateua na kuwafuta kazi maafisa wengi serikalini kama njia ya kutuliza ghadhabu za wananchi.

Duru za kuaminika katika nchi za magharibi na pia IMF zimesisitiza kuwa, pamoja na kuwa kwa muda mrefu Saudia imekuwa na pato kubwa la mafuta lakini haijaweza kuwawekea wananchi wake suhula bora za maisha na kwamba takribani asilimia 70 ya raia wa nchi hiyo wana maisha mabovu na hali mbaya ya kiuchumi.

Mbali na hayo, hali mbaya ya kibinadamu, ufisadi, uingiliaji kijeshi katika nchi jirani na kudorara uchumi ni mambo yanayaowakasirisha raia wa Saudia. Ni kwa msingi huu ndio maana katika miaka ya hivi karibuni kumeshuhudiwa maandamano kadhaa ya kutaka mabadiliko ya kimsingi hasa katika sekta za siasa na uchumi. Ili kuzima mwamko unaoendelea kuimarika wa wananchi watawala wa ukoo wa Aal Saud wanawafuta kazi baadhi ya maafisa wa ngazi za juu na kuwasilisha mipango iliyojaa hadaa.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …