Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatatu, 25 Aprili 2016 17:53

Matamshi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika mkutano na Rais wa Afrika Kusini

Matamshi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika mkutano na Rais wa Afrika Kusini
Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini ambaye Jumapili aliwasili Tehran akiongoza ujumbe wa ngazi za juu alikutana na kufanya mazungumzo na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika mkutano na Rais Zuma alisisitiza kuhusu udharura wa kuimarishwa ushirikiano miongoni mwa nchi huru na zinazojitegemea duniani.

Katika kikao hicho aliashiria nukta muhimu katika uhusiano wa Iran na Afrika Kusini. Awali ni hatua ya Iran kukata uhusiano wake mara moja na utawala wa ubaguzi wa rangi wa Makaburu wa Afrika Kusini mara baada ya kupata ushindi Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran na kusema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilikata uhusiano wake na utawala wa Kizayuni wa Israel na utawala wa ubaguzi wa rangi wa Afrika Kusini takriban kwa wakati mmoja. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amekumbushia nafasi muhimu ya hayati Nelson Mandela wa Afrika Kusini katika kuanguka utawala wa ubaguzi wa rangi nchini humo na historia yake nzuri, ya kiudugu na kimapenzi na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Nukta ya pili ambayo Kiongozi Muadhamu aliitaja ni kuwa, mtazamo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusu Afrika Kusini ni mtazamo mzuri na kubainisha kuwa, uhusiano wa Iran na Afrika Kusini ni mzuri sana. Ameongeza kuwa, ushirikiano wa nchi hizo mbili katika jamii za kimataifa pia unasaidia sana. Pamoja na hayo amesema, bado uwezo wa nchi hizi mbili haujatumiwa ipasavyo kwa ajili ya kukuza mabadilishano ya kiuchumi na kibiashara baina ya pande mbili.

Kwa upande wake Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini ameishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa uungaji mkono wake kwa wananchi wa nchi yake wakati wa mapambano na ubaguzi wa rangi na kusema kuwa, wananchi wa Afrika Kusini kamwe hawawezi kusahau uungaji mkono huo wa taifa la Iran kwao.

Katika hali ya sasa ya mfumo wa kimataifa, nchi huru na zinazojitegemea zinaweza kukidhi maslahi yao na hilo litategemea kiwango cha ushirikiano baina yao katika nyuga mbali mbali. Lakini pamoja na hayo, hakuna shaka kuwa kuna vizingiti katika njia ya ushirikiano huu. Hii ni kwa sababu madola makubwa ya kibeberu na kiistikbari kamwe hayataafiki ushirikiano kama huo ambao ni kwa madhara ya maslahi yao haramu.

Ni kwa sababu hii ndio baadhi ya madola makubwa kwa visingizio visivyokubalika, yanajaribu kuweka vizingiti katika uhusiano wa nchi huru na zinazojitegemea.

Iran na Afrika Kusini ni kati ya nchi zinazolengwa na njama hizo za madola ya kibeberu.

Uzoefu umeonyesha kuwa, ushirikiano ni kwa maslahi ya nchi zinazojitegemea. Moja ya misdaki za ushirikiano huo ni maingiliano mema ya Iran na Afrika Kusini katika Harakati ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote.

Afrika Kusini kwa mtazamo wa kisiasa na kiuchumi ni moja kati ya nchi muhimu na zenye taathira barani Afrika na inahesabiwa kuwa kati ya nchi zinazoibuka kiuchumi. Iran kwa upande wake pia ni nchi yenye uwezo mkubwa na hadhi ya kipekee katika uga wa kieneo na kimataifa na hivyo kushirikiana na Afrika Kusini kunaweza kuwa fursa nzuri kwa nchi hizo mbili.

Kwa hakika tunaweza kusema matamshi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na Rais wa Afrika Kusini ni ramani ya njia ya kufikiwa malengo ya pamoja ya Tehran na Pretoria.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …