Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatatu, 25 Aprili 2016 08:35

Kuasisiwa Daesh na Saudia kwa ridhaa ya CIA

Kuasisiwa Daesh na Saudia kwa ridhaa ya CIA
Ripoti iliyopewa jina la 'Daesh Mlelewa wa Wasaudi na CIA ina taarifa' imechapishwa tena na kuzidi kuakisiwa nchini Marekani na kugonga vichwa vya ripoti na habari.

Ripoti ya kukiri watawala wa Aal-Saudi nchini Saudia juu ya kuhusika kwao katika kuunda genge hilo, iliripotiwa kwa mara ya kwanza na gazeti la Kiingereza la Financial Times katika habari inayohusiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry. Katika ripoti hiyo, gazeti hilo la Financial Times liliandika kuwa, watawala wa Saudia walimueleza Kerry kuwa wao ndio walioliandaa kundi la Daesh na kwamba Shirika la Ujasusi la Marekani CIA lina taarifa juu ya suala hilo. Baada ya hatua ya gazeti hilo ripoti hiyo ilichapishwa tena na vyombo mbalimbali vya habari nchini Marekani. Aidha katika mazungumzo baina ya watawala wa Aa-Saud na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani walisisitiza kuwa, uingiliaji wa Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati, ndio ulioisukuma Riyadh kuanzisha makundi ya kigaidi ya al-Qaidah na Daesh. Watawala hao wa Saudia wanadai kuwa, mashambulio na uvamizi wa Marekani wa mwaka 2003 dhidi ya Iraq, ulibadilisha mahesabu kwa maslahi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, hivyo walilazimika kuchukua hatua za kukabiliana na suala hilo. Ronald Ernest Paul, mwandishi na mwanasiasa mashuhuri wa nchini Marekani na ambaye pia amewahi kuwa mwakilishi katika Kongresi ya nchi hiyo ameandika kuwa, wakati akizungumza na Daniel McAdams, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Ron Paul, alisema kuwa, kukiri watawala wa Saudia juu ya kuhusika kwao katika kuanzisha genge hilo la Daesh, si jambo la kushtusha. Kwa mujibu wa Ernest Paul, Saudia peke yake isingeweza kuanzisha genge hilo la kigaidi bila ya Shirika la Ujasusi la Marekani CIA kuwa na taarifa. Mwandishi huyo wa Marekani ameongeza kuwa, CIA na Wizara ya Ulinzi ya Marekani Pentagon, zilifanya njama nyingi baada ya kuanza mgogoro wa Syria kwa lengo la kutaka kumuondoa madarakani Rais Bashar al-Assad wa nchi hiyo na kwamba katika kutekeleza mradi huo, hakukuwa na budi isipokuwa kuanzishwa kundi la Daesh ambalo lilihitajika ili kutekeleza ajenda hiyo. Kwa kuzingatia kuwa Saudia ndio kitovu cha fikra za Uwahabi duniani, ilihusika moja kwa moja katika kuandaa makundi yenye misimamo ya kufurutu ada ambapo makundi hayo ya Kiwahabi na kwa majina tofauti yaliibuka na kujitangaza kwa mara ya kwanza nchini Syria. Kwa mfano tu, Saudia ndio iliyohusika moja kwa moja katika kuundwa kwa kundi la kigaidi la Taleban huko nchini Afghanistan. Kundi hilo lililopata mafunzo ya kijeshi kwa fedha za Saudia, hii leo na kwa mujibu wa Ronald Ernest Paul, wanachama wa genge hilo la Taleban ndio waliotoa mafunzo ya kufurutu ada kwa vijana wa kizazi kipya ambao sasa wamevalia mavazi ya Daesh huko nchini Iraq na Syria. Kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh lilitangaza uwepo wake nchini Iraq mwaka 2003 baada tu ya kuvamiwa nchi hiyo na Marekani, ingawa wakati huo lilikuwa likijulikana kwa jina lingine. Katika wakati huo, kiongozi mkuu wa genge hilo yaani Abubakar al-Baghdadi alikuwa akishikiliwa jela akiwa ni mfungwa mwanachama wa al-Qaidah mwenye misimamo ya kufurutu ada. Hata hivyo aliachiliwa huru kwa ushawishi wa Marekani. Baada ya kuondolewa madarakani utawala wa Baathi nchini Iraq, mabaki ya viongozi wa utawala huo wakaanzisha ushirikiano na wanachama wa Daesh kwa lengo la kutaka kuiondoa madarakani serikali mpya ya nchi hiyo. Harakati za wanachama wa Baathi kwa kushirikiana na genge hilo la Daesh, zinajiri kupitia fremu ya misaada kamili ya Marekani na Saudia nchini humo. Aidha kuondolewa kurasa 28 kwenye ripoti inayohusiana na mashambulizi ya Septemba 11 mwaka 2001 huko nchini Marekani, kunaonyesha nafasi ya moja kwa moja ya Saudia katika kuunga mkono ugaidi. Hata hivyo kutokana na ushirikiano wa karibu uliopo baina ya Washington na Riyadh serikali ya Marekani imepinga kufichuliwa na kuwekwa hadharani ukweli wa kuhusika watawala wa Aal-Saudi katika mashambulizi hayo. Inaelezwa kwamba, katika kurasa zilizoondolewa kwenye ripoti hiyo ya mashambulizi ya Septemba 11, jina la Shirika la Ujasusi la Marekani CIA lilikuwa limetajwa pia. Kwa hakika hatua hiyo inamuondolea shaka mtu yeyote juu ya kuhusika watawala wa Saudia katika hujuma hizo na halikadhalika kuwa na taarifa CIA juu ya harakati za Saudia katika eneo la Mashariki ya Kati na kuasisi kwake makundi ya kigaidi likiwemo kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …