Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumapili, 24 Aprili 2016 17:05

Kufungua mashtaka Harakati ya Kiislamu ya Nigeria dhidi ya serikali na jeshi la nchi hiyo

Kufungua mashtaka Harakati ya Kiislamu ya Nigeria dhidi ya serikali na jeshi la nchi hiyo
Harakati ya Kiislamu ya nchini Nigeria imeifungulia mashitaka serikali na jeshi la nchi hiyo kwa kuendelea kumshikilia kiongozi wa harakati hiyo, Sheikh Ibrahim Zakzaky kinyume cha sheria.

Sanjari na kubainisha suala hilo, Hassan Bala, mwanachama wa harakati hiyo ya Kiislamu amesema kuwa, ripoti iliyotolewa na serikali kuhusiana na jinai za hivi karibuni dhidi ya Waislamu wa Kishia wa nchi hiyo, ni ya kubuniwa na haina ukweli wowote. Kuhusu hali ya hivi sasa ya Sheikh Ibrahim Zakzaky, Bala amesema, jeshi la nchi hiyo limekataa kutoa maelezo yoyote juu ya hali ya kiongozi huyo pamoja na mke wake ambao hadi sasa wanaendelea kushikiliwa, suala ambalo limeifanya harakati hiyo ya Kiislamu kutokuwa na taarifa mpya kuhusu hali ya shakhsia hao. Ikiwa imepita miezi kadhaa tangu askari wa jeshi la Nigeria walipofanya mauaji ya mamia ya wafuasi wa harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo mwezi Disemba mwaka jana, wasi wasi umezidi kuongezeka kwa Waislamu wa nchi hiyo juu ya kufanyika ukandamizaji dhidi yao. Tarehe 12 na 13 za mwezi Desemba mwaka jana, jeshi la Nigeria lilifanya jinai ya kutisha katika makao makuu ya harakati hiyo ya Kiislamu mjini Zaria ambapo zaidi ya Waislamu 1000 wasio na hatia waliuawa. Kufuatia ripoti rasmi ya hivi karibuni ya Shirika la Msamaha Duniani la Amnesty International iliyolaani na kubainisha ukubwa wa jinai za jeshi la Nigeria dhidi ya Waislamu hao, kwa mara nyengine, hali ya Waislamu wa Kishia nchini humo imepewa mazingatio maalumu. Siku ya Ijumaa shirika hilo la msamaha duniani lilitoa ripoti na kutangaza kuwa, jeshi la nchi hiyo liliwaua kwa kuwapiga risasi kwa makusudi Waislamu 350, likawazika katika makaburi ya halaiki na kisha likafuta ushahidi na vielelezo vinavyohusiana na jinai hiyo. Kutolewa ripoti hiyo kumepokelewa kwa hisia na radiamali za kila upande japokuwa jeshi hilo limeipinga kwa kudai kuwa ni ya upande mmoja na iliyotolewa kwa pupa. Nigeria ni nchi ya magharibi mwa Afrika yenye idadi kubwa ya Waislamu katika eneo hilo. Kwa mujibu wa weledi wa mambo, katika kipindi cha miaka michache ya harakati za Kiislamu za Sheikh Ibrahim Zakzaky, kuliibuka wimbi la mwamko wa Kiislamu nchini humo na katika nchi jirani kiasi cha kuwavutia watu wengi kujiunga na harakati hiyo; suala ambalo liliwatia hofu viongozi wa Nigeria na maadui wengi wa Uislamu hata nje ya nchi hiyo. Katika upande mwingine baadhi ya nchi zimeanzisha harakati zao nchini Nigeria, na moja ya nchi hizo ni Saudia ambayo kutokana na kugonga mwamba sera zake katika eneo la Mashariki ya Kati, hivi sasa imeazimia kupenyeza ushawishi wake kwa Waislamu wa Afrika. Baadhi ya duru zimeripoti kuwa Saudia imedhamini silaha na fedha kwa ajili ya jeshi la nchi hiyo. Hayo yakiwa ni ya Saudia, kwa upande mwingine utawala haramu wa Kizayuni wa Israel nao haujabaki nyuma katika uwanja huo. Kuingilia masuala ya ndani na kadhalika kuwekeza katika sekta ya uchumi katika baadhi ya nchi za eneo la magharibi mwa Afrika, ni mambo ambayo yameongeza kiwango cha ushawishi na upenyaji wa Tel Aviv katika nchi hizo. Kabla ya hapo baadhi ya duru za habari ziliripoti kufanyika safari za siri za viongozi wa jeshi la Nigeria kuelekea Israel. Kwa mara kadhaa sasa jeshi la Nigeria limekuwa likituhumiwa kwa ufisadi, huku ufisadi huo ukijikita katika sekta mbalimbali. Kwa mujibu wa weledi wa mambo, jeshi la nchi hiyo na kwa kisingizio cha kupambana na kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram na sanjari na kujidhaminia silaha na uungaji mkono, limekuwa likitumia mwanya huo katika kuwahujumu Waislamu wa nchi hiyo. Mienendo hasi ya jeshi hilo inajiri katika hali ambayo kwa mara kadhaa, Rais Muhammadu Buhari amekuwa akisisitizia udharura wa kukabiliana na ufisadi sanjari na kufanya mabadiliko kadhaa jeshini. Inaonekana kuwa jeshi la Nigeria chini ya fremu ya kutafuta uungaji mkono wa nchi za kigeni na kujikusanyia misaada, limeamua kutekeleza ukandamizaji na mashinikizo dhidi ya Waislamu wa taifa hilo. Hivi sasa baada ya kutolewa ripoti ya Shirika la Msamaha Duniani la Amnesty International sambamba na hatua ya harakati ya Kiislamu kufungua mashitaka dhidi ya jeshi na serikali ya Abuja, jamii ya Waislamu wa wa Nigeria wanatumai kuwa hali ya Sheikh Ibrahim Zakzaky na mke wake itaweza kujulikana haraka na yeye kuweza kuachiwa huru pamoja na kuhitimishwa ukandamizaji na ukatili wa jeshi hilo dhidi ya Waislamu hao.../

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …