Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatano, 02 Machi 2016 06:17

Kuendelea harakati za kimataifa kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa Palestina

Kuendelea harakati za kimataifa kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa Palestina

Kuendelea hatua zisizo za kibinadamu za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina sambamba na kuendelea mzingiro dhidi ya Gaza na vile vile hujuma na uvamizi wa mara kwa mara wa utawala huo dhidi ya Ukanda wa Gaza unaofanyika kwa baraka za Marekani, kumelifanya eneo hilo kukabiliwa na hali mbaya mno ya kibinadamu.

Hatua ya Israel ya kulizingira eneo la Ukanda wa Gaza na kufanya mashambulio mtawalia dhidi ya eneo hilo kumelifanya eneo hilo kukabiliwa na maafa na kuifanya jamii ya kimataifa kuingiwa na wasiwasi mkubwa. Huu ni ukweli ambao umebainishwa wazi na wanaharakati wa kimataifa wa masuala ya amani ambao wametahadharisha pia kuhusiana na matokeo mabaya ya hatua hizo za Israel dhidi ya wananchi wa Palestina. Wanaharakati hao sasa wanafanya juhudi za kufikisha misaada yao huko Gaza ili kuonesha mshikamano wao na wakazi wa Gaza ambao wanakabiliwa na mzingiro. Ripoti zinasema kuwa, kumeongezeka harakati za kimataifa zenye lengo la kuwapelekea misaada ya kibinadamu wananchi wa Gaza na kwa muktadha huo kufanya juhudi za kuusambaratisha mzingiro huo na kuhitimisha machungu na masaibu wanayokabiliwa nayo wananchi hao wasio na hatia.

Hatua zilizo dhidi ya ubinadamu za utawala wa Kizayuni wa Israel haziishii tu katika mashambulio yake ya kiuwendawazimu, bali utawala huo bandia umekuwa ukitumia njia mbalimbali kama mzingiro katika maeneo ya Wapalestina hususan Ukanda wa Gaza lengo likiwa ni kuwauwa zaidi Wapalestina.

Kutokana na kushadidi mzingiro wa Israel huko Gaza katika miaka ya hivi karibuni mamia ya Wapalestina wamepoiteza maisha yao na hii ni katika hali ambayo idadi kubwa ya Wapalestina hususan wagonjwa wanakabiliwa na hatari ya kifo jambo ambalo linaonesha kuendelea mauaji ya Israel dhidi ya wakazi wa Gaza.

Kuendelea kushuhudiwa radiamali dhidi ya mzingiro wa Gaza kwa njia tofauti kama maandamano ya kulaani mzingiro huo katika nchi mbalimbali zikiwemo za barani Ulaya sambamba na juhudi za walimwengu za kuwafikishia misaada wananchi wa Gaza bila kusahau tangazo la kuiwekea vikwazo Israel ni jambo linaloonesha kushtadi ghadhabu na hasira za fikra za waliowengi ulimwenguni dhidi ya jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel. Akthari ya madola ya Ulaya ambayo daima yamekuwa muungaji mkono wa utawala wa Kizayuni, filihali yanaandamwa na fikra za waliowengi katika nchi zao. Nchi nyingi za Ulaya zimekuwa zikipiga kura kwa maslahi ya wananchi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa hususan kuhusiana na haki za Wapalestina likiwemo suala la haki ya taifa hilo madhulumu ya kujianishia mustakbali wake, haki ya kuundwa nchi huru ya Palestina na kuinuliwa nafasi ya taifa hilo katika umoja huo. Matukio hayo katika miaka ya hivi karibuni yanaonesha kubadilika siasa za nchi za Ulaya kutoka katika kuunga mkono utawala wa Kizayuni wa Israel na kufanya harakati za kuunga mkono haki za wananchi wa Palestina. Hii ni katika hali ambayo, wigo wa taathira za vikwazo dhidi ya Israel haujaishia tu katika engo ya siasa na kutengwa kisiasa, bali taathira hizo zimechukua mkondo mpana pia katika uchumi wa utawala huo vamizi. Wachambuzi wa masuala ya Israel wanasema kuwa, kiwango cha hasara katika sekta ya uchumi iliyotokana na vikwazo dhidi ya utawala huo inafikia zaidi ya dola bilioni nane kwa mwaka ambapo pigo hilo kubwa linatokana na utegemezi wa uchumi wa Israel kwa ulimwengu wa Magharibi.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …