Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Ijumaa, 09 Novemba 2012 11:08

Sisitizo la Rais wa Syria la kutothubutu taifa lolote la Magharibi kuishambulia nchi yake

Sisitizo la Rais wa Syria la kutothubutu taifa lolote la Magharibi kuishambulia nchi yake

Sambamba na kuendelea kwa njama za Wamagharibi za kuzusha visingizio mbalimbali kama njama za kutafuta njia za kuingilia kijeshi nchini Syria, Rais Bashar al-Assad wa nchi hiyo ametoa onyo kali kwa madola hayo kuwa, kushambuliwa kijeshi taifa lake kutazusha moto dunia nzima. Rais wa Syria aliyasema hayo jana Alkhamisi katika mahojiano na televisheni ya Rusia Alyaum katika radiamali yake dhidi ya njama zinazofanywa na baadhi ya nchi hususan Qatar, Saudi Arabia, Marekani na Uturuki za kutaka kuingilia kijeshi katika nchi hiyo ya Kiarabu na kuongeza kuwa, uingiliaji wowote wa kijeshi nchini Syria utahatarisha amani ya dunia nzima kwa ujumla. Aidha rais wa Syria amesisitiza kuwa, ikiwa taifa lolote litathubutu kuishambulia nchi yake, basi taifa la Syria litajibu hujuma hiyo kwa uwezo wake wote, suala ambalo litahatarisha usalama wa dunia nzima. Ameongeza kuwa, matatizo yatakayotokea Syria yatapelekea kuzuka kwa janga la Domino na kuenea katika maeneo tofauti ya dunia, kuanzia eneo la Bahari ya Atlanki hadi Bahari ya Pasifiki. Aidha ameashiria kuwa Syria ni ngome ya mwisho yenye kudhamini usalama na uthabiti wa eneo la Mashariki ya Kati na kusema kuwa, katu ulimwengu hauwezi kuhimili madhara ya kushambuliwa eneo nyeti kama hilo. Itakumbukwa kuwa hivi karibuni Waziri Mkuu wa Uingereza David William Cameron alitaka Rais wa Syria ang'oke madarakani jambo ambalo wachambuzi wa mambo wanasema hayonyesha ni kiasi gani viongozi wa nchi za Magharibi walivyo na kiburi na jinsi wanavyoyadharau mataifa mengine ya dunia. Kwa upande wake Rais wa Syria amesema katika mahojiano hayo kuwa yeye ni raia wa Syria na ataendelea kuishi Syria hadi mwisho wa uhai wake na kwamba wananchi wa Syria pekee ndio walio na haki ya kuamua waongozwe na nani na waishi kwenye maisha ya namna gani. Kwa upande mwingine Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Syria Faisal al-Miqdad jana Alkhamisi alilaani chokochoko za Marekani na waitifaki wake nchini Syria na kuongeza kuwa, Marekani ilipata pigo kali nchini Iraq na Afghanistan na kwamba hivi sasa Washington haina ubavu wowote wa kuanzisha vita na nchi yoyote ile duniani na kilichobakia hivi sasa ni kuendesha vita vya kisaikolojia tu dhidi ya mataifa yasiyokubaliana na siasa zake za kibeberu. Faisal al-Miqdad amekosoa vikali pia propaganda za vyombo vya habari vya Magharibi na uungaji mkono wao kwa makundi ya kigaidi nchini Syria akisema kusema, Magharibi na vibaraka wao wananyamazia jinai zinazotendwa na makundi ya kigaidi nchini humo.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …