Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumanne, 10 Februari 2015 10:30

Picha za ndege mpya ya kijeshi ilotengezwa na Iran

Picha za ndege mpya ya kijeshi ilotengezwa na Iran

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo imezindua ndege mpya ya kivita katika siku ya nane ya sherehe za al-Fajiri 10 za kuadhimisha ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu hapa nchini

Ndege hiyo ambayo ni kizazi kipya cha ndege ya kivita ya Swaiqah, imeundwa na wataalamu wa Wizara ya Ulinzi ya Iran. Naibu Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Jenerali Amir Hatami, amesema kuwa ndege ya Swaiqah-2, imeundwa kwa ubunifu mpya sanjari na kuongezwa uwezo na bora wake. Ameongeza kuwa, ndege hiyo inaweza pia kutoa mafunzo kwa marubani ili waweze kutumia ndege za kisasa za kivita. Akiashiria mwenendo wa Wizara ya Ulinzi wa kuimarisha ndege zake za kivita kwa kutegemea wataalamu wa ndani ya nchi, Hatami amesema kuwa ndege hiyo ya Swaiqah-2 ni ishara ya uwezo wa hali ya juu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika uga wa anga.

Ndege ya kivita ya Swaiqah ambayo ilianza kutumiwa na jeshi hapa nchini mwaka 2006 ni ya pili kutengenezwa na wataalamu wa Iran na inaweza kufuatilia ndege za kivita za adui, kushiriki katika mashambulizi, kulenga shabaha katika ardhi na kubeba shehena ya aina mbalimbali za silaha.

Ingia hapa chini kupata picha zaidi za ndege hiyo

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …