Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatano, 04 Juni 2014 13:00

Mashindano ya Kimataifa ya 31 ya Qur'ani Tukufu ya mjini Tehran

Mashindano ya Kimataifa ya 31 ya Qur'ani Tukufu ya mjini Tehran

Mashidano ya 31 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yamemalizika leo hapa Tehran bada kuendelea kwa muda wa wiki moja. Mashindano hayo yalianza tarehe 27 Rajab katika mkesha wa maadhimisho ya kubaathiwa Mtume Muhammad SAW.  Mashindano hayo yalikuwa na maqarii na mahufadh 120 wa Qur'ani Tukufu kutoka nchi 75 duniani huku kukiwa na jopo la majaji 15 ambapo 10 kati yao ni kutoka nchi za kigeni na watano ni Wairani.  Kulikuwa na washiriki kadhaa kutoka nchi za Afrika Mashariki ambapo mshiriki kutoka Tanzania ameshika nafasi ya tano katika qiraa. Makundi yote mawili ya hifdhi na qiraa yalikuwa na washindi watano kila moja. Katika upande wa Qiraa mshindi alikuwa Ja'afar Fardi kutoka Iran huku nafasi ya pili ikishikwa na Mohammad Asghari kutoka Ufilipino akifuatiwa na Mahmoud Mohammad Yusuf Misri naye Sayyid Thamaruddin Samaddof kutoka Tajikistan ameshika nafasi ya nne huku Ustadh Mohammad Ramadhani Iddi  kutoka Tanzania akishika nafasi ya tano. Katika kiwango cha hifdhi Behzad Hizhbery kutoka kutoka Iran ameshika nafasi ya kwanza akifuatiwa na Abdulqadir Abdul Aziz Ahmad Abdul Aziz kutoka Misri naye Mutiullah Mutmain kutoka Afghanistan amepata nafasi ya tatu ambapo Mohammad Lotfi Suleiman wa Indonesia ameshika nafasi ya nne huku Haroun Mamadou Hassan wa Niger akishika nafasi ya tano. Washindi wote wamemtunukiwa zawadi ya Qur'ani Tukufu, Cheti cha Shukrani, nishani na kitita cha fedha. Ustadh Mohammad Ramadhani Iddi  kutoka Tanzania amezungunza na Radio Tehran akiwa katika mashindano. Bonyeza hapa kusikiliza mahojiano hayo.

Tumeorodhesha hapa chini baadhi ya picha za mashindano hayo.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …