Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumamosi, 10 Mei 2014 12:08

Mjumuiko wa visiwa 1864, kila kisiwa kina nyumba moja

Mjumuiko wa visiwa 1864, kila kisiwa kina nyumba moja

Mjumuiko wa visiwa 1864 vilivyoko kwenye mpaka wa Canada na Marekani katika mto wa St Lawrence unachora picha nzuri sana ya kimaumbile na kuonesha utukufu wa Allah aliyewaumbia wanadamu dunia yenye sura za kuvutia inayoweza kukalika na kuwamiminia humo neema Zake nyingi sana viumbe Wake mbalimbali.

Ukubwa wa eneo la visiwa hivyo 1864 unakadiriwa kuwa ni zaidi ya meli mraba 40 na wenyeji wake wakuu ni ndege wa majini wanaohama-hama.

Kisiwa kikubwa zaidi kati ya visiwa hivyo kinajulikana kwa jina la Wolfe chenye urefu wa kilomita 29 na upana wa kilomita 9.

Mwaka 2002 eneo linalojumuisha visiwa hivyo lilitangazwa na UNESCO kuwa ni hifadhi ya kimataifa.

Aghlabu ya visiwa hivyo havikaliwi na watu na mara nyingi utapata nyumba moja katika kila kisiwa na wakazi wake wanatumia boti kwenda na kurudi bara.

Nyumba za visiwa hivyo zinatumia umeme wa maji na huduma za simu zinatumia nyaya zilizowekwa chini ya maji kutoka kisiwa kimoja hadi kingine.

Ametukuka Allah, Mbora wa kuumba.

Hapa chini tumeorodhesha baadhi ya picha za visiwa hivyo.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …