Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumanne, 26 Aprili 2016 10:17

Askofu Mkuu wa Ufaransa alalamikia maudhi ya ngono dhidi ya watoto

Askofu Mkuu wa Ufaransa alalamikia maudhi ya ngono dhidi ya watoto

Askofu Mkuu wa mji wa Lyon nchini Ufaransa amesema kuwa kuteuliwa makasisi wasiofaa ndiyo sababu inayopelekea kuongezeka kwa vitendo vya ufisadi na maudhi ya ngono dhidi ya watoto nchini humo.

Kwa mujibu wa gazeti linalochapishwa nchini humo la Le Figaro, Kadinali Philippe Barbarin, Askofu Mkuu wa mjini Lyon alitoa taarifa hapo jana Jumatatu akitangaza kuwa kuna makosa makubwa yanayofanyika wakati wa kuteuliwa makasisi. T

aarifa hiyo imetolewa baada ya kufanyika kikao cha faragha kilichowajumuisha makasisi wapatao 200 kwa madhumuni ya kuchunguza kesi zinazowahusisha baadhi ya makasisi wanaofanya uhalifu wa kuwabaka watoto wadogo nchini humo. Taarifa hiyo imesema kuwa makasisi wamefanya makosa na uzembe mkubwa katika utekelezaji wa majukumu yao. Baadhi ya makasisi wanakubaliana na hatua ya Kadinali Philippe Barbarin kutaka kujiuzulu alihali wengine wanasisitiza juu ya kufuatiliwa kisheria kesi za ubakaji wa watoto kwenye vyombo vya mahakama vya Ufaransa.

Mahakama moja ya mjini Lyon imepokea malalamiko ya familia mbili zilizoathirika na uhalifu huo wa makasisi dhidi ya watoto wao na kuanzisha uchunguzi kuhusiana na suala hilo. Imewakosoa vikali viongozi wa Kanisa Katoliki la Lyon akiwemo Kadinali Philippe Barbarin kwa kutotoa habari mapema kuhusiana na uhalifu huo kwa vyombo vya mahakama.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)