Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumanne, 19 Aprili 2016 21:04

Wito wa kukabiliana na propaganda chafu dhidi ya Uislamu Marekani

Wito wa kukabiliana na propaganda chafu dhidi ya Uislamu Marekani
Kituo cha Kiislamu cha America Kaskazini kimetoa wito wa kukabiliana na wimbi la propaganda chafu dhidi ya Uislamu.

Mamia ya wanachama wa Kituo cha Waislamu cha Amerika Kaskazini waliokuwa Washington huko Marekani wameitaka Congresi ya nchi hiyo kukabiliana na wimbi kubwa la kuchafua sura na jina la Uislamu na dhulma za kijamii nchini Marekani.

Mkurugenzi wa Kituo cha Kiislamu cha America Kaskazini, Naeem Beg amesema kuwa kituo hicho kimekuwa chini ya mashinikizo makubwa kutokana na kushadidi wimbi la propaganda chafu dhidi ya Uislamu na kwamba sababu yake ni kejeli na madharau ya wanasiasa wa Marekani dhidi ya Uislamu.

Beg amesema wawakilishiwa Congresi ya Marekani wanapaswa kuelewa kwamba, hawakuchaguliwa kwa ajili ya kufanya mashinikizo na kushirikiana na Wall Street, bali wajibu wao ni kushughulikia matakwa watu aliowapigia kura.

Mkurugenzi wa Kituo cha Kiislamu America Kaskazini amesema makundi na jumuiya nyingi zenye mitazamo ya kufurutu mipaka zinaendesha shughuli zao nchini Marekani na zinapiga vita Uislamu.

Hali hiyo ya wimbi la propaganda chafu dhidi ya Uislamu na Waislamu nchini Marekani imeshadidi zaidi kutokana na matamshi na hujuma zinazofanywa na wanasiasa kama Donald Trump na Ted Cruz wanaowania tiketi ya kugombea kiti cha rais wa Marekani wka tiketi ya chama cha Republican.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)