Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumapili, 17 Aprili 2016 12:14

Mtetemeko mkubwa wa ardhi waikumba Ecuador, watu 77 wanaripotiwa kufariki dunia

Mtetemeko mkubwa wa ardhi waikumba Ecuador, watu 77 wanaripotiwa kufariki dunia
Viongozi wa Ecuador wametangaza kuwa, watu wasiopungua 77 wamefariki dunia kufuatia mtetemeko mkubwa wa ardhi ulioikumba nchi hiyo.

Ripoti za awali zinasema kuwa, tetemeko hilo la ardhi lilikuwa na ukubwa wa 7.8 kwa kipimo cha rishta. Rais Rafael Correa wa Ecuador ametangaza hali ya hatari baada ya kutokea zilzala hiyo na ametoa mkono wa pole kwa familia zilizopoteza ndugu zao kufuatia janga hilo la kimaumbile.

Habari zinasema kuwa, tetemeko hilo la ardhi liliyoyakumba maeneo ya kaskazini magharibi mwa Ecuador limesababisha hasara kubwa.

Serikali ya Ecuador imewataka wananchi kuondoka katika maeneo ya pwani ya kaskazini magharibi mwa nchi hiyo na kwenda katika maeneo ya miinuko, baada ya kuweko taarifa za uwezekano wa kutokea mawimbi ya Tsunami katika baadhi ya maeneo ya pwani ya nchi hiyo.

Shughuli za uokoaji zinaendelea huku kukiweko na uwezekano wa kuongezeka idadi ya watu waliopoteza maisha kufuati tetemeko hilo la ardhi kutokana na majengo mengi kuporomoka katika maeneo yaliyokumbwa na janga hilo la kimaumbile.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)