Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatatu, 11 Aprili 2016 08:56

Sanders akosoa mashambulizi ya Israel dhidi ya watu wa Gaza

Sanders akosoa mashambulizi ya Israel dhidi ya watu wa Gaza
Mgombea tiketi ya chama cha Democratic kwa ajili ya kinyang'anyiro cha uchaguzi wa rais nchini Marekani, Bernie Sanders amekosoa vikali mashambulizi ya mwaka 2014 ya utawala haramu wa Israel dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza.

Pamoja na kutangaza uungaji mkono wake kwa Israel, Sanders ameyataja mashambulizi ya utawala huo ghasibu dhidi ya watu wa Gaza hapo mwaka 2014 kuwa hayakuwa sahihi na kutoa wito kwa serikali ya Marekani kuwa na siasa zenye uadilifu katika eneo la Mashariki ya Kati.

Bernie Sanders mbaye yeye mwenyewe ni Myahudi amesema, iwapo hatutaamilia kwa heshima na Wapalestina haitawezekana kupatikana amani katika eneo la Mashariki ya Kati.

Wapalestina wasiopungua 2200 wakiwemo watoto wadogo 577 waliuawa shahidi katika mashambulizi ya kinyama ya siku 50 yaliyofanywa na Isarel mwaka 2014 dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)