Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Ijumaa, 08 Aprili 2016 18:36

Nato na Russia huenda zikaanzisha mazungumzo baada ya miaka miwili

Nato na Russia huenda zikaanzisha mazungumzo baada ya miaka miwili
Russia imesema kuwa huenda ikafanya mazungumzo na Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi Nato katika wiki chache zijazo.

Russia imesema kuwa huenda ikafanya mazungumzo na Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi Nato katika wiki chache zijazo hiyo ikiwa ni mara ywa kwanza tangu uhusiano wa pande mbili hizo uingie dosari mwaka 2014 kutokana na mgogoro wa Ukraine. Alexey Mshekov Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema leo kuwa Baraza la Nato na Russia linataraji kuitisha mkutano baada ya karibu miaka miwili.

Jumatano wiki hii, Jens Stoltenberg Katibu Mkuu wa Muungano wa Nato alisema kuwa muungano huo wa nchi za Magharibi uko katika mchakato wa majadiliano na maafisa wa Russia ili kufikia mapatano kuhusu wanachotaka kuzungumza na kisha ndipo waitishe mkutano.

Katibu Mkuu wa Nato amesema muungano huo hautaki kuzozana na Russia na kwamba utajiepusha na vita baridi vipya. Itakumbukwa kuwa Baraza la Russia na Nato liliundwa mwaka 2002 lengo likiwa ni kuanzisha jukwaa la mazungumzo kuhusu masuala ya kiusalama kati ya Russia na nchi wanachama wa Nato.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)