Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Ijumaa, 08 Aprili 2016 12:52

Wairaqi: US inaunga mkono ugaidi, Daesh

Wairaqi: US inaunga mkono ugaidi, Daesh

Utafiti mpya wa maoni umeonyesha kuwa thuluthi moja ya wananchi wa Iraq wanaamini kuwa Marekani ndiyo muungaji mkono mkubwa wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh.

Ripoti ya utafiti huo uliofanywa na Idara ya Masuala ya Nje ya Marekani imebainisha kuwa, mmoja kati ya kila Wairaqi watatu wanaitakidi kuwa serikali ya Washington inaunga mkono ugaidi na ukatili unaofanywa na matakfiri wa Daesh haswa nchini Iraq. Aidha ripoti hiyo imebainisha kuwa, asilimia 40 ya Wairaqi walioshirikishwa kwenye utafiti huo uliofanywa kati ya Oktoba na Novemba mwaka jana wanaamini kuwa Marekani inaiunga mkono Daesh ili kuvuruga siasa na usalama wan chi hiyo kwa lengo la kudhibiti rasimimali zake.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa, kiwango cha Wairaqi kuichukia Marekani kimeongezeka kutoka asilimia 18, Disemba mwaka 2014 hadi asilimia 38 Agosti mwaka jana.

Wakati huo huo matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanywa na shirika la Rasmussen Reports yanaonesha kuwa asilimia 58 ya Wamarekani wanapinga uingiliaji wa serikali yao katika nchi za Kiislamu kwa kisingizio cha kueneza demokrasia. Ripoti ya shirika hilo imeashiria uvamizi wa kijeshi wa Marekani dhidi ya Iraq na kueleza kuwa wataalamu wengi wa sera za nje za Washington wanaamini kwamba sera hizo ndizo zilizosababisha kujitokeza kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh (ISIL) na makundi mengine ya kigaidi.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)