Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumamosi, 02 Aprili 2016 12:19

Obama: Ni kweli ‘drones’ zetu zimeua raia

Obama: Ni kweli ‘drones’ zetu zimeua raia

Rais Barack Obama wa Marekani amekiri kuwa ndege zisizo na rubani za nchi hiyo zimeua idadi kubwa ya raia wasio na hatia katika nchi mbali mbali duniani na hususan za Kiislamu.

Obama aliyasema hayo jana katika Kongamano la Usalama wa Nyuklia mjini Washington na kuongeza kuwa, Marekani inabeba dhima ya vifo vya raia wasio na hatia katika hujuma zake za drone katika nchi za Libya, Syria, Somalia na kwengineko.

Rais wa Marekani amejitetea kuwa serikali yake hata hivyo imechukua hatua za makusudi za kupunguza mauaji ya raia katika hujuma za ndege zisizokuwa na rubani za nchi hiyo.

Shirika la Kijasusi la Marekani CIA limekuwa likitumia ndege hizo kutekeleza hujuma na ujasusi katika nchi za Afghanistan, Pakistan, Somalia, Yemen na Syria kwa kisingizio cha kukabiliana na makundi ya kigaidi.

Ikulu ya White House ya Marekani kwa mara ya kwanza mwezi uliopita ilisema hivi karibuni itatoa takwimu za watu waliouawa katika hujuma za drone za Marekani tangu mwaka 2009.

 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)