Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Alkhamisi, 31 Machi 2016 18:48

Waziri wa Ufaransa alazimika kuomba radhi baada ya kukejeli hijabu

Waziri wa Ufaransa alazimika kuomba radhi baada ya kukejeli hijabu
Waziri wa Haki za Wanawake wa Ufaransa amejikuta pabaya baada ya kutoa matamshi ya kuwavunjia heshima wanawake wa Kiislamu na vazi la stara la hijabu.

Laurence Rossignol amelazimika kuwaomba radhi wanawake wa Kiislamu nchini humo kwa kuwafananisha na watu weusi waliokubali kufanywa watumwa nchini Marekani. Katika mahojiano na kanali ya televisheni ya BMF na idhaa ya RMC nchini Ufaransa hapo jana, waziri huyo aliyakejeli matamasha yanayowaruhusu wanamitindo waliovalia mavazi ya stara kama burqa samba na kufunika mikono na miguu yao na kusema kuwa hatua hiyo ni ya kipumbavu.

Muda mfupi baada ya kutoa kauli hizo za kibaguzi na dharau, maelfu ya wanaotumia mitandao ya kijamii walimkashifu na kumtaka aombe radhi kwa matamshi yake hayo. Katika muda wa masaa machache, sahihi zaidi ya elfu 10 zilikuwa zimekusanywa katika ukurasa mmoja wa mitandao ya kijamii kumshinikiza waziri huyo ajiuzulu kutokana na kauli yake ya kibaguzi. Baadaye Rossignol alilazimika kuomba radhi na kusema kuwa 'ulimi uliteleza' kutokana na matamshi hayo ya kibaguzi.

Chuki dhidi ya Waislamu na Uislamu barani Ulaya zimeongezeka kwa asilimia 275, tangu baada ya shambulizi la Paris lililofanywa na kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh na kusababisha watu zaidi ya 130 kuuawa na mamia ya wengine kujeruhiwa mwishoni mwa mwaka jana 2015.

Mbali na Ulaya, baadhi ya viongozi wa kisiasa nchini Marekani kama vile Donald Trump, mgombea tiketi ya chama cha Republican kwa ajili ya kinyang'anyiro cha uchaguzi wa rais nchini Marekani, wamekuwa wakitoa kauli za chuki dhidi ya Waislamu katika kampeni zao.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)