Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Alkhamisi, 31 Machi 2016 07:05

Obama: Waislamu ni wahanga wa ugaidi

Obama: Waislamu ni wahanga wa ugaidi
Rais Barack Obama wa Marekani amekiri kwamba Waislamu ni wahanga wa ugaidi.

Obama ambaye alikuwa kihutubia katika shughuli za kidini mjini Washington amesisitiza kuwa Wakristo na Waislamu wamekuwa wahanga wa ugaidi na kwamba lengo la magaidi ni kudhoofisha imani za watu na kueneza chuki na mtazamo mbaya kuhusu dini na mbari tofauti.

Obama ameongeza kuwa mashambulizi ya kigaidi yanawashawishi Wamarekani wawafukuze watu wanaotafuta hifadhi.

Matamshi hayo ya Rais Barack Obama akikiri kwamba Waislamu na Wakristo ni wahanga wa ugaidi yametolewa wakati Marekani na washirika wake wamekuwa wakiyaunga mkono na kuyafadhili kwa misada ya kifedha na kijeshi makundi ya kigaidi kama Daesh ambayo yanafanya jinai za kutisha katika nchi kama Iraq na Syria.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)