Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatano, 30 Machi 2016 20:30

Wazayuni wachangia kunyanyaswa Waislamu US

Wazayuni wachangia kunyanyaswa Waislamu US

Imam wa Msikiti wa al-Islam mjini Washington, Marekani amesema serikali ya nchi hiyo na Wazayuni wana muelekeo wa pamoja na wanashrikiana katika kuwakandamiza Waislamu wa nchi hiyo.

Sheikh Abdul-alim Musa, amesema serikali za Democrats na Republicans kwa kushirikiana na Wazayuni wenye ushawishi wameukandamiza sana Uislamu na Waislamu nchini Marekani na kwamba mwenendo huo ungali unaendelea.

Imam wa Msikiti wa al-Islam mjini Washington ameeleza kuwa Waislamu wamekabiliwa na mashambulio ya moja wa moja ya Wazayuni wa Kimarekani wenye satua na ushawishi.

Kwa mujibu wa Sheikh Abdul-alim Musa, kaulimbiu za kampeni zinazotolewa na wagombea wa uteuzi wa kuwania urais wa Marekani zimeilenga jamii ya Waislamu.

Aidha amesema makundi makubwa ya kutetea haki za kiraia nchini Marekani yamenyamaza kimya na wala hayatetei haki za Waislamu.

Donald Trump, ambaye anaongoza miongoni mwa wanaowania kuteuliwa kugombea urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican, wiki iliyopita alirudia tena kauli yake ya kutaka Waislamu wasiruhusiwe kuingia nchini humo.

Seneta Ted Cruz na wagombea wengine wa uteuzi wa kuwania urais kwa tiketi ya chama cha Republican, nao pia wametaka hatua kali za usalama zichukuliwe katika maeneo wanayoishi Waislamu nchini humo.../

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)