Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Ijumaa, 19 Februari 2016 07:09

Huffington Post: Maelfu ya wanawake wa Canada waliuawa

Huffington Post: Maelfu ya wanawake wa Canada waliuawa

Gazeti la Marekani la The Huffington Post limeripoti kuwa idadi ya wanawake asilia wa Canada waliouawa au kutoweka ni kubwa zaidi ya takwimu zilizokadiriwa hapo awali.

Huffington Post imeandika kuwa maafisa wa serikali ya Canada wametangaza kuwa, takwimu zilizotolewa kuhusu wanawake asilia wa nchi hiyo ni kubwa zaidi ya ile iliyotolewa hapo awali.

Uchunguzi uliofanyika umebaini kuwa, zaidi ya wanawake wakazi asili wa Canada waliotoweka au kuuliwa ni zaidi ya elfu 4,200.

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch mwaka 2013 lilitoa ripoti ya kina kuhusu jinsi wanawake hao wakazi asili wa Canada walivyokuwa wakipigwa na kunyanyaswa. Wanawake na wasichana wakazi wa asili wa Canada wanaunda asilimia nne ya watu wa jamii ya nchi hiyo.

Waziri Mkuu mpya wa Canada, Justin Trudeau alitangaza baada ya kushinda uchaguzi kwamba atafanya uchunguzi kuhusu mauaji na kutoweka kwa maelfu ya wanawake wakazi asilia wa nchi hiyo.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)