Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumapili, 27 Septemba 2015 09:06

Wajerumani waunga mkono mazungumzo na Asad

Wajerumani waunga mkono mazungumzo na Asad

Vyama mbalimbali nchini Ujerumani vimekaribisha pendekezo la hivi karibuni la Kansela wa nchi hiyo Bi Angela Merkel kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Rais wa Syria ili kuupatia ufumbuzi mgogoro wa nchi hiyo. Cem Ozdemir Mkuu wa chama cha Kijani cha Ujerumani ameunga mkono msimamo wa Kansela wa nchi hiyo kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Rais Bashar Assad na kueleza kuwa, iwapo kufanya mazungumzo na Assad kutasaidia, basi Berlin inapasa kutekeleza jambo hilo. Ozdemir amesema pia kuwa Russia na Iran zinapasa kushirikishwa katika mazungumzo hayo. Naye Volker Kauder mkuu wa mrengo wa vyama vya Kikristo vya Ujerumani amesisitiza kuwa mashambulizi ya anga dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh hayatoshi; na kwamba mashambulizi ya nchi kavu pia yanapaswa kutekelezwa dhidi ya kundi hilo. Ursula von der Leyen Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani amesisitiza kuwa kunapaswa kwa uchache kuweko muafaka wa kisiasa na Russia katika kikao cha Umoja wa Mataifa, ili kutuliza mapigano huko Syria. Huko nyuma, baadhi ya wabunge wa Ujerumani pia walitaka kuzidishwa uungaji mkono wa kijeshi wa nchi hiyo katika mapambano dhidi ya Daesh.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)