Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Alkhamisi, 24 Septemba 2015 09:16

Russia yatishia kujibu mapigo ya Marekani

Russia yatishia kujibu mapigo ya Marekani

Russia imeitahadharisha Marekani kuhusu mpango wake wa kupeleka mabomu 20 ya kisasa ya nyuklia kwenye kituo chake cha kijeshi nchini Ujerumani.

Msemaji wa Ikulu ya ya Rais wa Russia Kremlin, Dmitry Peskov amesema hatua hiyo itavuruga mlingano wa kistratijia barani Ulaya na utajibiwa kwa hatua za kurejesha mlingano huo. Msemaji wa Kremlin ameongeza kwamba hiyo ni hatua nyingine hatari ya kuzidisha mivutano barani Ulaya. Amesema hatua hiyo haiwezi kuimarisha utulivu, kujenga imani na kuimarisha usalama barani Ulaya.

Msemaji wa ikulu ya Rais wa Russia hakusema ni hatua gani zitakazochukuliwa na Moscow iwapo Marekani itatekeleza azma yake ya kupeleka mabomu ya kisasa ya nyuklia kwenye kambi yake huko Ujerumani lakini shirika la habari la Interfax la Russia limenukuu maafisa wa jeshi la nchi hiyo wakisema kuwa yumkini Russia ikajibu hatua hiyo kwa kupeleka makombora yake mapya ya nyuklia ya Iskander-M katika eneo la Kaliningrad huko Ulaya mashariki kwenye mipaka ya nchi za Poland na Lithuania.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)