Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatano, 23 Septemba 2015 09:05

Le Pen kupelekwa kizimbani kwa kuwatusi Waislamu

Le Pen kupelekwa kizimbani kwa kuwatusi Waislamu

Vyombo vya mahakama za Ufaransa vimetangaza kuwa kiongozi wa chama cha National Front (FN), Marine Le Pen atapandishwa kizimbani tarehe 20 Oktoba kujibu mashtaka ya kutoa matamshi ya kichochezi dhidi Waislamu.
Disemba mwaka 2010 katika kampeni za uchaguzi za chama chake, Marine Le Pen alisema kuwa Swala za Waislamu wa Ufaransa mitaani ni sawa na uvamizi wa manazi dhidi ya Ufaransa wakati wa Vita vya Pili vya Dunia. Alisisitzia kuwa Swala na ibada ya Waislamu ni uvamizi dhidi ya Ufaransa lakini bila ya vifaru na wanajeshi.
Matamshi hayo ya kibaguzi ya kiongozi wa chama cha tatu kwa ukubwa cha siasa nchini Ufaransa yaliwakasirisha sana Waislamu na jumuiya za kupinga ubaguzi ambazo ziliwasilisha mashtaka mahakama. Vilevile Bunge la Ulaya liliondoa kinga ya kushtakiwa Marine Le Pen na hivyo kufungua mlango wa kufikishwa mahakamani mwanasiasa huyo mbaguzi wa Ufaransa.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)