Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatatu, 21 Septemba 2015 20:30

EU yakaribisha ushindi wa Alexis Tsipras Ugiriki

EU yakaribisha ushindi wa Alexis Tsipras Ugiriki

Siku moja baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa nchini Ugiriki, viongozi mbalimbali wa Ulaya wanaendelea kumpongeza Alexis Tsipras, kiongozi wa chama cha mrengo wa kushoto cha Syriza kwa kuibuka na ushindi. Umoja wa Ulaya umetoa taarifa na kumpongeza Tsipras kwa ushindi wake na kusema uko tayari kushirikiana na serikali yake mpya. Wagiriki walishiriki katika uchaguzi mkuu wa mapema hapo jana ulioitishwa na Tsipras baada ya baadhi ya wabunge wa chama chake kuasi na kupinga sera zake bungeni. Ingawa kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 41 ameshinda katika uchaguzi huo lakini hakuweza kupata idadi ya viti vinavyotakiwa ili kuunda serikali na kwa mantiki hiyo atalazimika kuunda serikali ya muungano. Tayari ametangaza kuwa atashirikiana na chama cha mrengo wa kulia cha 'Independent Greeks' kinachoongozwa na Panos Kammenos katika kuunda serikali hiyo. Tsipras alikabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa chama cha New Democracy ambacho kimejipatia asilimia 29 ya kura zilizopigwa. Ugiriki ambayo imekuwa na matatizo makubwa ya kiuchumi imeshaongozwa na serikali 6 na kushuhudia chaguzi nne za ubunge katika kipindi cha miaka 7 iliyopita.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)