Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumapili, 13 Septemba 2015 14:59

Maandamano ya Ulaya kuunga mkono wahajiri

Maandamano ya Ulaya kuunga mkono wahajiri

Maandamano makubwa yamefanyika katika nchi kadhaa za Ulaya kuwaunga mkono wahajiri wanaomiminika katika nchi hizo. Idadi kubwa ya Wajerumani wamejitokeza barabarani kukaribisha wahajiri kutoka nchi kadhaa za dunia, wengi wao wakiwa ni kutoka Syria. Nchini Uingereza waandamanaji wameitaka serikali itekeleze wajibu wake wa kimataifa katika kuwapokea na kuwalinda wahajiri. Maandamano ya aina hiyo pia yameshuhudiwa katika nchi za Italia, Uhispania na Austria.

Nchini Poland wananchi ambao kwa kawaida huwa na misimamo ya kufurutu ada dhidi ya Wageni na Uislamu wamepinga nchi yao kuwapokea wahajiri huku wakibeba mabango yenye jumbe dhidi ya Uislamu.

Mgogoro wa wahajiri umeshadidi mno katika siku za hivi karibuni ambapo nchi za Ulaya zimekuwa zikipokea makumi ya maelfu ya wahajiri kutoka Eritrea, Sudan, Libya na Syria.

Russia imesema sera mbaya za kigeni za nchi za Ulaya ndio sababu kuu ya kutokea mgogoro huo wa wahajiri. 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)