Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatano, 09 Septemba 2015 20:42

Russia: Marekani inavuruga vita dhidi ya ugaidi

Russia: Marekani inavuruga vita dhidi ya ugaidi

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia, sanjari na kukosoa mienendo hasi ya Marekani katika kupambana na ugaidi amesema kuwa, siasa za Washington katika uwanja huo ni zenye madhara. Maria Zakharova, ameyasema hayo leo katika kikao na waandishi wa habari na kuongeza kuwa, Marekani haishirikiani na nchi zinazopambana na magenge ya kigaidi, na kwamba suala hilo linadhihirisha ni namna gani Washingtona ilivyo na undumakuwili katika vita hivyo. Amesisitizia umuhimu wa ushirikiano wa jamii ya kimataifa katika kupambana na kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh, huku akiikosoa vikali Marekani kwa kutokuwa jaddi katika vita vyake dhidi ya kundi hilo. Aidha Zakharova ameashiria juu ya umuhimu wa kuzisaidia nchi zinazopambana na magenge hayo ya kigaidi hususan Daesh na ameitaka Washington kufungamana na misingi ya kimataifa sanjari na kushirikiana na Syria katika uwanja huo. Amesema kuwa, ushirikiano wa Russia na Marekani katika masuala mengi umezidi kuzorota kutokana na miamala hasi ya Washington na kwamba suala hilo limechangia kukosekana ushirikiano wa kutosha katika mapambano dhidi ya ugaidi. Amekosoa propaganda za vyombo vya habari vya Magharibi juu ya kuwepo askari wa Russia nchini Syria na kuongeza kuwa, ni washauri wa masuala ya kijeshi pekee wa nchi hiyo ndio  walioko Syria. Amesema kazi ya washauri hao ni kutoa ushauri wa kijeshi  tu kwa jeshi la Syria juu ya matumizi ya silaha na si vinginevyo.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)