Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumamosi, 05 Septemba 2015 20:40

'Nchi za Ulaya ‘lazima zichukue wakimbizi laki mbili’

'Nchi za Ulaya ‘lazima zichukue wakimbizi laki mbili’

Nchi za Umoja wa Ulaya lazima zikubali kuwapa hifadhi wakimbizi laki mbili kama sehemu ya ‘stratijia ya pamoja’ ya kukabiliana na mgogoro wa wakimbizi duniani. Hiyo ni kauli ya mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) Antonia Guterres ambaye amezitaka nchi za Umoja wa Ulaya kutumia nguvu zao zote kutatua mgogoro uliopo.

Hayo yamejiri wakati amapo leo maelfu ya wakimbizi kutoka Hungary wameingia nchi jirani ya Austria. Aghalabu ya wakimbizi hao ambao ni kutoka Syria wanatazamiwa kuelekea Ujerumani. Austria imesema wakimbizi 6,000 wameingia nchini humo na wengine wengi wanatarajiwa kuwasili katika kile kinachotajwa kuwa na mgogoro mkubwa zaidi wa wakimbizi barani Ulaya tokea vita vya Yugoslavia katika muongo wa 1990. Ulaya inakabiliwa na wimbi kubwa zaidi la wakimbizi ambapo watu 300,000 wakiwa wameyaweka maisha yao hatarini kuvuka Bahari ya Mediterenia, na kueleka katika nchi za bara hilo mwaka huu pekee. Wakimbizi hao ni kutoka nchi za Afrika na Mashariki ya Kati. Zaidi ya watu 2,600 wamefariki dunia wakijaribu kuvuka bahari hiyo, akiwemo mtoto Msyria aitwaye Aylan Kurdi aliyekuwa na umri wa miaka mitatu, ambaye picha ya maiti yake akiwa amelala pwani nchini Uturuki baada ya kusomwa na maji, imeibua huzuni kubwa katika nyoyo za watu kote duniani.

Rais Vladimir Putin wa Russia amesema mgogoro huo wa wakimbizi umesbabishwa na sera mbovu za Umoja wa Ulaya kuingilia mambo ya ndani ya nchi za Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)