Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumapili, 14 Februari 2016 10:39

Mashambulio ya Saudia yaua makumi ya raia Yemen

Mashambulio ya Saudia yaua makumi ya raia Yemen

Watu 15 wameuawa na makumi ya wengine wamejeruhiwa katika mashambulio ya anga yaliyofanywa alfajiri ya kuamkia leo na ndege za kivita za utawala wa Aal Saud katika mji wa kale na wa kihistoria wa Kaukaban ulioko mkoani Al Mahwit magharibi mwa Yemen.

Aidha watu kadhaa wameuawa na kujeruhiwa katika shambulio jengine la ndege za kivita za Saudia lililolenga na kuteketeza kikamilifu viwanda kadhaa katika eneo la Shuub katika mji mkuu wa Yemen, Sana'a.

Mashambulio ya anga ya majeshi vamizi ya utawala wa Aal Saud na waitifaki wake yamebomoa msikiti na nyumba kadhaa pamoja na kuharibu mashamba katika mji wa Sarwah mkoani Ma'rib katikati mwa Yemen. Inasemekana kuwa zaidi ya raia 10 wameuawa katika shambulio hilo.

Katika kujibu mashambulio na jinai za utawala wa Aal Saud, jeshi la Yemen na vikosi vya wananchi vimewaangamiza wanajeshi kadhaa wa Saudia katika shambulio dhidi ya askari hao katika mji wa Al Rabuu'ah katika eneo la Usair nchini humo.

Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu limesema linatiwa wasiwasi na mauaji ya kikatili dhidi ya raia wa Yemen na kutangaza kuwa misaada ya tiba iliyopelekwa kwenye baadhi ya maeneo ya nchi hiyo ukiwemo mkoa wa kusini wa Taiz haitoshi hata kidogo. Watu wapatao laki mbili wanakabiliwa na hatari ya kifo mkoani humo kutokana na uhaba wa suhula za tiba.../

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)