Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Ijumaa, 12 Februari 2016 19:23

Wanajeshi Wayemen waua askari 20 Wasaudia Jizan

Wanajeshi Wayemen waua askari 20 Wasaudia Jizan
Askari wasiopungua 20 wa Saudi Arabia wameuawa katika katika eneo la Jizan kusini magharibi mwa ufalme huo katika mapigano na wanajeshi wa Yemen.

Katika taarifa, Wizara ya Ulinzi ya Yemen imesema wanajeshi hao wameuawa walipojaribu kulidhibiti tena eneo la kistratijia la Jabal al Doud mkoani Jizan leo Ijumaa.

Kanali ya Televisheni ya al-Masirah imeongeza kuwa jeshi la Yemen limevurumisha kombora katika uwanja mmoja wa ndege huko Jizan.

Kwingineko katika mkoa wa Ma'rib ndani ya Yemen, vikosi vya nchi kavu vya Yemen vimekabiliana vikali na wanajeshi vamizi wa Saudia katika wilaya ya Sarvah huku ndege za kivita za Saudia zikidondosha mabomu katika maeneo ya magharibi mwa mkoa huo. Katika mji wa pili kwa ukubwa Yemen, Aden, wanamgambo sita watiifu kwa rais mtoro wa nchi hiyo Abd Rabbu Mansur Hadi wameuawa katika mapigano yaliyojiri katika eneo la al Basateen leo Ijumaa.

Yemen imekuwa ikishambuliwa na jeshi la Saudia na waitifaki wake tokea mwezi Machi mwaka jana kwa lengo la kumrejesha madarakani rais mtoro wa nchi hiyo Abdu Rabbu Mansur Hadi ambaye ni kibaraka wa utawala wa Riyadh.

Takwimu zainaonesha kuwa katika hujuma za kinyama za Saudia dhidi ya Yemen, watu karibu 8,400 wameuawa wengi wakiwa ni raia hasa watoto na wanawake. Idadi ya watoto Wayemeni waliouawa katika hujuma za Saudia ni 2,236. Aidha Saudia imedondosha mabomu katika mahospitali, misikiti, shule, viwanda, madaraja na miundombinu yote ya Yemen. Saudia pia inatumia mabomu yaliyopigwa marufuku katika hujuma zake za kuogofya dhidi ya wananchi wa Yemen.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)