Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatano, 03 Februari 2016 06:49

"Mwaka 2016 ni mwaka wa Jeshi na wananchi Yemen"

"Mwaka 2016 ni mwaka wa Jeshi na wananchi Yemen"

Mkuu wa Kamati Kuu ya Mapinduzi ya Yemen amesisitiza kuwa, mwaka 2016 ni mwaka wa jeshi la nchi hiyo kwani limethibitisha ushujaa, ukakamavu, nguvu na muqawama wake mbele ya adui.

Shirika la habari la ISNA limemnukuu Muhammad Ali al Houthi akisema hayo na kuongeza kuwa, Wizara ya Ulinzi wa Yemen inafanya jitihada za kuendesha ratiba maalumu za kuunda upya muundo wa baadhi ya vikosi vyake hususan vikosi vya kulinda baraza la uongozi.

Al Houthi ameongeza kuwa, vikosi vya ulinzi vya Yemen ndiyo nguzo kuu ya usalama na kulinda ardhi yote ya nchi hiyo na vimejiandaa kikamilifu kupambana na wakoloni na kuwafurusha nje ya mipaka ya Yemen.

Mkuu wa Kamati Kuu ya Mapinduzi ya Yemen ameongeza kuwa: Vita vilivyoanzishwa dhidi ya Yemen na dhidi ya uhuru wa nchi hiyo, ni vita vya kinyama na visivyokubalika hata kidogo ambavyo mamluki kutoka kila pembe ya dunia wamekusanyika pamoja kufanya ukatili na mauaji nchini humo.

 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)