Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatatu, 01 Februari 2016 06:25

Wanajeshi wa Saudi Arabia waendelea kuangamizwa

Wanajeshi wa Saudi Arabia waendelea kuangamizwa

Wanajeshi zaidi ya 200 wa Saudia wameuawa na magari na zana za kijeshi za nchi hiyo kuharibiwa vibaya katika shambulio lililofanywa na jeshi la Yemen katika kituo cha anga cha al Anad kusini mwa Yemen.

Habari zinasema kuwa, mamluki wengi wa Saudia waliokuweko kwenye kambi hiyo walikuwa ni wanajeshi wa Sudan.

Kwa mara ya kwanza jeshi la Sudan limethibitisha kuuliwa mwanajeshi wake mmoja huko Yemen. Ahmad Khalifa al Shami msemaji wa jeshi la Sudan ndiye aliyetangaza habari hiyo. Sudan ilijiunga na muungano vamizi dhidi ya Yemen unaoongozwa na Saudi Arabia tangu mwezi Oktoba mwaka jana.

Saudi Arabia ilianzisha vita dhidi ya wananchi wa Yemen tangu mwezi Machi mwaka jana, na imekuwa ikishambulia kwa ndege za kivita maeneo mbalimbali ya raia wa Yemen, na kuuwa maelfu ya watu wasio na hatia kwa kisingizio cha kutaka kumrejesha madarakani Rais aliyetoka nchi wa Yemen.

Shambulio la jeshi la Yemen na makundi ya kujitolea ya raia wa nchi hiyo katika kambi ya kijeshi ya al Anad limesababisha pia kuuliwa Nicolaus Petros kamanda wa Kimarekani aliyekuwa akiongoza kikosi chenye uhusiano na shirika la Black Water katika kambi ya al Anad kusini mwa Yemen.

 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)